BUKOBA SPORTS

Saturday, September 14, 2013

ENGLAND PREMIER LEAGUE: SUNDERLAND 1 vs ARSENAL 3, AARON RAMSEY ANG'ARA AFUNGA BAO MBILI, GIROUD AKIFUNGA MOJA HUKO STADIUM OF LIGHT!!

SUNDERLAND 1 vs ARSENAL 3
Aaron Ramsey ameifungia Arsenal Bao 2 walipoitandika Sunderland Bao 3-1 huko Stadium of Light.
Mchezaji mpya wa Arsenal, Mesut Ozil, ambae alicheza vizuri, ndie aliempa pasi Olivier Giroud kufunga Bao la Dakika ya 11 lakini Sunderland walisawazisha kwa Bao la Penati ya Craig Gardner katika Kipindi cha Pili. 

Lakini baada ya Ramsey kufunga Bao la Pili kwa Arsenal, Refa Martin Atkinson alileta utata mkubwa pale Jozy Altidore alipomtoka Bacary Sagna na kufunga Bao lakini Refa huyo aliashiria kuwa Sagna alicheza Faulo kabla Bao kufungwa na kuwaacha Sunderland wakilalamika kwanini Bao halikubaki.
Hata hivyo, Ramsey akafunga Bao la 3 na kuwanyamazisha Sunderland na kuipa Arsenal ushindi wa Bao 3-1.
Aaron Ramsey akishangilia na  Kieran Gibbs baada ya kufunga bao Craig Gardner akishangilia baada ya kufunga mkwaju wa penati hapaCraig Gardner akichonga penati kumfunga kipa wa Gunners Wojciech SzczesnyMeneja wa Sunderland  Paolo Di Canio akilalamikia moja wapo ya bao la utata!!Jozy Altidore na Bacary Sagna wakigombea mpira hapaTheo Walcott kwenye patashikaMchezaji mpya wa Arsenal Mesut Ozil akigombea mpira hapa na  Ki Sung-Yeung wa Sunderland
Olivier Giroud akifurahi na Mesut Ozil baada ya kuipatia bao  ArsenalJack WilshereMesut Oezil wa Arsenal akichuana na Valentin Roberge wa Sunderland
VIKOSI:
Sunderland (4-2-4): Westwood 7; Celustka 6, Diakite 5, Roberge 6, Colback 6; Vaughan 5 (Gardner 46, 8) Ki 6; Johnson 7, Fletcher 6 (Wickham 77), Altidore 6, Mavrias 5 (Borini 72, 6).
Subs not used: Brown, Larsson, Cuellar, Mannone.
Goal: Gardner 48 (pen)
Booked: Gardner.
Arsenal (4-2-3-1): Szczesny 6; Jenkinson 7, Sagna 6, Koscielny 7, Gibbs 7; Flamini 7, Wilshere 7; Ozil 9 (Vermaelen 80), Ramsey 8, Walcott 6 (Monreal 88); Giroud 7 (Akpon 90+3).
Subs not used: Frimpong, Miyaichi, Akpon, Gnabry, Fabianski. Booked: Flamini, Sagna.
Goals: Giroud 11, Ramsey 67, 76.
Referee: Martin Atkinson 5
Att: 39.055


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi 14 Septemba
Man United 2 Crystal Palace 0
Aston Villa 1 Newcastle United 2
Fulham 1 West Bromwich Albion 1
Hull City 1 Cardiff City 1
Stoke City 0 Manchester City 0
Sunderland 1 Arsenal 3
Tottenham Hotspur 2 Norwich City 0
19:30 Everton 1 v Chelsea 0* unaendelea kipindi cha 1 kimeisha.


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumapili 15 Septemba
18:00 Southampton v West Ham United
Jumatatu 16 Septemba
22:00 Swansea City v Liverpool

No comments:

Post a Comment