Bao la kwanza lilifungwa na Robin van
Persie kwa Penati ya Dakika ya 46 iliyotolewa baada ya Mchezaji kutoka
Afrika Kusini Kagisho Dikgacoi kumchezea Rafu Ashley Young iliyomfanya
Mchezaji huyo mbali ya kusababisha Penati pia kutolewa nje kwa Kadi
Nyekundu.
Mchezaji mpya wa Man United, Marouane Fellaini, aliingizwa katika Dakika ya 62 na kupokelewa na shangwe kubwa.
Wayne Rooney, ambae alicheza Mechi hii
huku amejifunga kinga usoni kufunika Jeraha alilopata Wiki mbili
zilizopita, aliifungia Man United Bao la pili katika Dakika ya 81 kwa
Frikiki murua iliyopanda juu ya ukuta na kushuka Golini na kumshinda
Kipa Speroni.
Mechi inayofuata ya Ligi Kuu England kwa
Man United ni Jumapili ijayo Septemba 22 huko Uwanja wa Etihad dhidi ya
Mahasimu wao wakubwa Manchester City.
Lakini, kabla ya hapo, Jumanne watakuwa Old Trafford kucheza Mechi ya Kundi A la UEFA CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Bayer Leverkusen.
Wayne Rooney akifurahia na kupongezwa na wenzake baada ya kuipachikia bao la pili United dakika ya 81
Rooney akiachia shuti kali
Marouane Fellainina Marouane Chamakh kwenye kashikash za kuutafuta mpira
Mchezaji mpya wa Man United, Marouane Fellaini, aliingizwa katika Dakika ya 62 na kupokelewa na shangwe kubwa. Na hapa alikuwa akiusindikiza mpira kuelekea goli la Crystal Palace.
Wayne Rooney chupuchupu aliukosa mpira hapa kwa klosi safi ya Robin van Persie
Robin van Persie akiachia shuti kali wakati anapiga penati dakika za mwishoni kipindi cha kwanza
Majanga:Ashley Young akiangushwa chini eneo hatari la penati na Kagisho Dikgacoi
Wayne Rooney akikabwa na Adrian Mariappa
Anderson wa Manchester United kwenye patashika na Jason Puncheon wa Crystal Palace
Marouane Fellaini alianzia benchi kwenye mtanange huu kabla ajaingia kipindi cha pili
Sir Alex Ferguson nae alikuwa mmoja wa watazamaji leo hii Old Trafford
Sir Alex Ferguson akiutazama mtanange
Baadhi ya Mashabiki walivaa nywele za Bandia kwenye uwanja wa Old Trafford kufanana na Fellaini ikiwa ni ishara ya kumkaribisha
Kipute kamili!!!!
Old Trafford walimkaribisha vilivyo Fellaini baadhi kwa kuvaa wigi!!
No comments:
Post a Comment