
Kocha wa Everton Roberto Martinez (kushoto) akisalimiana na kocha wa Newcastle mapema kabla ya mtanange kuanza.

Viongozi: Hapa anaonekana Newcastle director of football Joe Kinnear (katikati) akicheki mtanange wa ugenini uwanja wa Goodison Park leo hii wakicheza na Everton

Kocha wa Everton Roberto Martinez akicheki vijana wake usiku huu wakati wanamenyena na Newcastle United.
Everton leo wameendeleza ubabe wa kutofungwa kwao tangu msimu huu uanze walipoifunga timu ya
Newcastle mabao 3-0 kipindicha kwanza kwenye uwanja wao wa Goodison
Park. Mabao ya Everton yamefungwa na Lukaku dakika ya tano, bao la pili
likafungwa na Ross Barkley dakika ya 25 na bao la dakika ya 37
likifungwa tena na Romelu Lukaku na hatimaye kipindi cha kwanza
kikamalizika 3-0 dhidi ya Newcastle.
Romelu Lukaku (Katikati) akiwapatia bao la mapema Everton dakika ya tano

Lukaku akishangilia bao lake kwa kuifungia timu yake mpya ya Everton dhidi ya Newcastle.
Kipindi cha pili Newcastle waliingia kwa ubabe na hamu ya kutaka kurudisha mabao hayo, Dakika ya 51 mchezaji Yohan Cabaye akaachia shuti kali na la mbali na kwenda moja kwa moja nyavuni na kujipatia bao nakufanya 3-1.
Kocha wa Newcastle akishangaa mabao hayo matatu ya kipindi cha kwanza na kuwaza jinsi ya kuyarudisha!!

Lukaku akimfunga kipa wa Newcastle Tim Howard bao

Lukaku akawapachikia bao lingine na kufanya 3-0 dhidi ya Newcastle.
No comments:
Post a Comment