Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, akiongea wakati wa hafla ya chakula cha jioni ilioandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuchangisha fedha kufanikisha kampeni ya “Dawati kwa kila mtoto” inayoendeshwa na taasisi hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bank M, Bw.Nimrod Mkono(MB) akisikisiliza kwa makini kwenye hafla hiyo ambapo zaidi ya Shilingi Milioni 200 zilichangishwa kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo wakati wa chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kununulia Madawati kwa shule za msingi nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba, Dr. Salim Ahmed Salim pamoja na Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhani.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Wairoba pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Majaar Trust Balozi Mwanaidi Majaar wakati wa hafla ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kampeni ya “Dawati kwa kila mtoto” inayoendeshwa na taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba na Dr. Salim Ahmed Salim wakielekea kwenye meza ya chakula.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Hawa Ghasia (kulia) akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhani.
Mwenyekiti wa Taasisi ya HMT Balozi Mwanaidi Maajar akiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali kupakua chakula cha jioni kilichoandaliwa na taasisi hiyo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla ya hiyo wakibadilishana mawazo.
Mkongwe wa Muziki nchini John Kitime akitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment