Marafiki waungana: Mshambuliaji mpya wa Chelsea Samuel Eto'o anajivunia kufanya kazi tena na Jose Mourinho.
Samuel Eto'o ametanabaisha kuwa aliwahi kumchukia Jose Mourinho siku za nyuma kabla ya kuanza kuwa naye katika kikosi cha timu ya taifa ya Inter Milan.
Mourinho mnamo 2009/2010 aliifanya Inter kuwa ni timu ya kutetemesha na alifanya hivyo akiwa sambamba na Eto'o ambaye alikuwa katika kiwango cha kuvutia ambaye alisajiliwa kama mbadala wa Zlatan Ibrahimovic.
'Kabla ya kukutana Inter, hatukuwa tukijuana kila mmoja, hivyo mahusinao yetu yalikuwa magumu,' Eto'o amekaririwa na gazeti la The Sun.
'Sikuwahi kusema itafika siku kwamba nitakuja kuchezea klabu inatakayofundishwa na Jose.
'Lakini mungu anajua zaidi. alitaka kunionyesha kuwa nilikuwa na makosa. Sasa ni kocha wangu tena.'
Eto'o amejiunga na Chelsea kwa ada ya pauni milioni £7 akitokea katika klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi katika siku za mwisho za uhamisho wa wachezaji baada ya klabu hiyo kushindwa kumpata Wayne Rooney.
Kumekuwa na wakati mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Cameroon amekuwa akituhumiwa kwa matatizo kadhaa kiasi kuchangia kuondoka Barca mwaka 2009 lakini akiwa Inter, chini ya Mourinho dhamira yake ilikuwa wazi kuelekea katika mafanikio.
Eto'o alihusishwa kutaka kujiunga na Chelsea wakati huo klabu hiyo ikisaka mshambuliaji mwaka 2006 ambapo Adriano alikuwa katika mpango kama huo kabla ya Andriy Shevchenko kusajiliwa kwa ada ya pauni milioni £30.
Walikuwa katika kipindi cha mafanikiwa enzi hizo wakiwa Italy katika klabu ya Inter Milan.
Mafanikio ya kutisha: Inter ilishinda ligi ya mabingwa Ulaya na taji la ligi mwaka 2009/2010 wakati huo Mourinho na Eto'o wakiwa pamoja.
No comments:
Post a Comment