Monday, September 16, 2013

KESHO JUMANNE HAPATOSHI! UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MANCHESTER UNITED v BAYER 04 LEVERKUSEN.

LEO JUMANNE Usiku UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, inaanza kwa Mechi 8 za Makundi A hadi D na ndani ya hizo ni ile ya Mabingwa Watetezi Bayern Munich ambao wako Nyumbani kucheza na Warusi CSKA Moscow.
Old Trafford itashuhudia Mechi ya Mabingwa wa England Manchester United kucheza na Klabu ya Germany, Bayer 04 Leverkusen, huku wenzao Man City wako Ugenini huko Czech Republic kucheza na FC Viktoria Plzeň.
Mechi nyingine za Jumanne ambazo zinahusu Klabu maarufu ni zile za huko Uturuki wakati Galatasaray wataminyana na Real Madrid, huko Denmark ni FC Copenhagen na Juventus wakati Ugiriki ni Olympiacos dhidi ya Paris Saint-Germain.

Marouane Fellaini akijifua kwa ajili ya mtanange mkali wa kesho Manchester United wakati watakapocheza na Bayer 04 Levelrkusen.
Kwenye mazoezi jana

Wayne Rooney alionekana nae akijifua na wenzake




RATIBA:
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku]
Jumanne 17 Sep 2013
Manchester United FC v Bayer 04 Leverkusen
Real Sociedad de Fútbol v FC Shakhtar Donetsk
Galatasaray A.Åž. v Real Madrid CF
FC København v Juventus
SL Benfica v RSC Anderlecht
Olympiacos FC v Paris Saint-Germain
FC Bayern München v PFC CSKA Moscow
FC Viktoria Plzeň v Manchester City FC
Wayne Rooney
Rooney
Rooney na Nemanja Vidic wakifanya mazoezi

Meneja mpya David Moyes akifurahishwa na mazoezi ya wachezaji wake Manchester United kwenye mazoezi yao ambapo kwa kocha huyu yatakuwa kwa mara ya kwanza

Shinji Kagawa akiteta na kocha wake David Moyes baada ya kipindi kirefu kupita tangu Community Shield

MANCHESTER UNITED FC v BAYER 04 LEVERKUSEN
Hii ni mara ya 18 mfululizo kwa Man United kushiriki kampeni za UCL lakini kwa Meneja wao mpya, David Moyes, hii ni mara ya kwanza kwake kucheza Hatua ya Makundi ya Mashindano haya ambayo Klabu yake imeyatwaa mara 3.
Vile vile, Kwa Meneja wa Bayer Leverkusen, Sami Hyypia, hii ni mara ya kwanza kuongoza Timu kwenye UCL lakini ameshawahi kutwaa Ubingwa akiwa Mchezaji wa Liverpool Mwaka 2005.
Timu hizi zimewahi kucheza mara 4 kwenye UCL.

MECHI ZILIZOPITA:
13/11/02 Man United 2 Bayer 04 Leverkusen 0 [UCL, Makundi]
24/09/02 Bayer 04 Leverkusen 1 Man United 2 [UCL, Makundi]
30/04/02 Bayer 04 Leverkusen 1 Man 1 [UCL, Nusu Fainali]
24/04/02 Man United FC 2 Bayer 04 Leverkusen 2 [UCL, Nusu Fainali]

Kocha David Moyes amejionea mwenyewe jitihada za veteran defender Rio Ferdinand akisakata kabumbu

Moyes akiwaangalia wachezaji wake Van Persie, Nani (katikati) na Cleverlykulia wakifanya mazoezi

Veteran Ryan Giggs alionekana nae akifanya mazoezi hapa

Robin van Persie akifanya mazoezi ambaye anategemewa sana kucheza kesho

RATIBA JUMATANO UEFA CHAMPIONS
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku]
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 04 v FC Steaua BucureÅŸti
Chelsea FC v FC Basel 1893
Olympique de Marseille v Arsenal FC
SSC Napoli v Borussia Dortmund
FK Austria Wien v FC Porto
Club Atlético de Madrid v Football Club Zenit
AC Milan v Celtic FC
FC Barcelona v AFC Ajax

No comments:

Post a Comment