BUKOBA SPORTS

Friday, September 6, 2013

KINARA ANDY MURRY ANG'OLEWA NA STANISLAS WAWRINKA US OPEN 2013.


Andy Murray
Mcheza Tennis Andy Murray amepoteza kofia ya ubingwa wa US Open katika mchezo huo baada ya kukubali kuupoteza ubingwa huo hiyo jana mikononi mwa kijana raia wa Uswizi anayekuja kwa kasi Stan Wawrinka.
Murray alipokutana na vyombo vya habari alikiri mchezo ulikuwa mgumu na kujikuta akiangukia pua safari hii katika michuano ya wazi nchini Marekani ijulikanayo kama US Open 2013. Wawrinka
Mara zote Murray amekuwa akijituma vilivyo ili kushinda katika michuano hiyo tangu michuano ya Wimbledon ya miezi miwili iliyopita.
Murray hakujaribu kujitetea kufuatia kubwagwa na Wrawinka ambapo alimsifia mpinzani wake huyo kwa kufanya mashambulizi yaliyomtoa kwa kipigo cha seti 6-4,6-3,6-2. 
Wawrinka akijipongeza

Mashabiki upande wa Murray

No comments:

Post a Comment