Australia, ambao wamefuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia Mwakani Nchini Brazil wakitokea Kanda ya Asia pamoja na Japan, South Korea na Iran, walizidiwa kila kitu kwenye Mechi hii.
Brazil walianza kufunga Bao zao katika Dakika ya 8 wakati krosi ya Neymar ilipounganishwa na Bernard na shuti lake kupiga posti na kumaliziwa na Jo.
Kazi nzuri ya Mkongwe Maicon, akiichezea Brazil baada ya kukosekana kipindi kirefu, ilimfungulia njia Bernard ambae krosi yake iliunganishwa vyema na Jo aliefunga Bao lake la pili na la pili kwa Brazil.
Mchezaji wa Barcelona Neymar akimfunga kipa Mark Schwarzer bao la tatu
Hadi Mapumziko, Brazil 3 Australia 0.
Ramires alifunga Bao la 4 kwa kichwa katika Dakika ya 57 alipounganisha krosi ya Fulbeki Maxwell alieingizwa badala ya Marcelo.
Dakika ya 72 Alexandre Pato aliifungia Brazil Bao la 5 baada ya ushirikiano mzuri wa Hernanes, alieingia Kipindi cha Pili, na Neymar.
Luiz Gustavo alifunga Bao la 6 kwa kigongo kikali katika Dakika ya 83 na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Nchi yake.
Jumanne Septemba 10, Brazil itacheza Mechi nyingine ya Kirafiki na Portugal huko Gilette Stadium, Boston, Massachusettes, Marekani.
Mchezaji wa Chelsea Ramires akifunga tena bao la nne
Mchezaji Alexandre Pato alitokea benchi na kuifungia bao la tano Bazil
No comments:
Post a Comment