MENEJA wa Germany Joachim Low ameuelezea
uamuzi wa Real Madrid kumuuza Mesut Ozil kwa Arsenal ni kitu
kisichoeleweka huku Wachezaji wa Real, akiwemo Cristiano Ronaldo,
wakihuzunika na kuondoka kwake.
Jumatatu Usiku, Siku ya mwisho ya
Kipindi cha Uhamisho, Arsenal ilivunja Benki na Rekodi yao wenyewe kwa
kutoa Kitita cha Pauni Milioni 42.4 kumnunu Kiungo huyo wa Germany mara
tu baada ya Real kumsaini Gareth Bale kwa Dau la Rekodi ya Dunia la
Pauni Milioni 86.
Ozil kushoto akionesha jezi ya Gunners juu na kulia ni Straikar Lukas Podolski
Mesut Ozil
-Katika Misimu mitatu na Real Madrid, Ozil alisuka Bao 47 kwenye La Liga na yeye kufunga Bao 19.
-Katika Misimu mitatu na Real Madrid, Ozil alisuka Bao 47 kwenye La Liga na yeye kufunga Bao 19.
Lakini Meneja wa Germany Joachim Low amehoji uamuzi wa kumruhusu Ozil kuihama Real.
Amesema: “Kwangu, haieleweki kwa Real
kumuuza mmoja wa Wafungaji wao bora. Wachezaji wengi wa Real kama Sami
Khedira na Cristiano Ronaldo wamehuzunika na Uhamisho huu.”
Hata hivyo, Kocha huyo wa Germany
amegusia kuwa Ozil atanufaika na kuhamia Arsenal kwa jinsi Meneja wa
Klabu hiyo, Arsene Wenger, alivyohangaika kumsaini.
Low, ambae yuko na Ozil kwenye Kikosi
cha Germany ambacho Ijumaa kinapambana na Austria kwenye Mechi ya Kombe
la Dunia, amedai sapoti ya Wenger na staili ya uchezaji ya Arsenal
itamsaidia sana Mchezaji huyo.
Nao Wachezaji wa Real wameibuka na kuzungumza kwa huzuni kuhusu Uhamisho wa Ozil.
Nyota wao mkubwa, Cristiano Ronaldo,
alitamka: “Yeye alikuwa ndie Mchezaji mkubwa aliejua muvu zangu
Uwanjani. Nimekasirika kuondoka kwake!”
Nae Sergio Ramos alisema: “Ni mwenzangu
na Rafiki yangu! Ni aibu. Ni Mchezaji bora. Ingekuwa naamua nini
kinatokea Real, angekuwa Mtu wa mwisho kuondoka!”
Si Wachezaji tu waliohuzunishwa kuhusu
Ozil, hata aliekuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Real, Jorge Valdano,
amesema: “Kama wangenipa mimi uamuzi, ningeweka mbele ushirikiano wa
Ozil-Angel Di Maria kuliko Bale. Hakika ningemweka Ozil mbele ya Bale!”
Sergio Ramos nae kaanika tisheti iliyoandikwa mgongoni Ozil kwenye Twitter
Isco amekuwa mchezaji mwingine aliyeumia kuuzwa kwa mchezaji huyo!!!
Ozil ameuzwa baada ya Real Madrid kununua Jembe Bale kwa £86million kutoka Tottenham
Ozil akitoa pasi wakati wanacheza na timu ya Granada kushoto ni Brayan Angulo na Hassan Yebda
No comments:
Post a Comment