
Mario Balotelli, akizuiliwa na mchezaji mwenzake Marco Amelia baada ya kupewa kadi nyekundu
MENEJA wa klabu ya AC Milan, Massimiliano Allegri amemuonya Mario Balotelli kujifunza kufunga mdomo wake baada ya nyota huyo kupewa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ambapo Milan walichapwa mabao 2-1. Katika mchezo huo Balotelli alikosa penati yake ya kwanza katika maisha yake ya soka la kulipwa na baadae kujikuta akipokea kadi ya pili ya njano kwa kuzozana na mwamuzi baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa. Alegri amesema akama mchezo umekwisha ni vizuri ukanyamaza kwani kuzozana na mwamuzi hakuwezi kubadilisha mchezo inabidi ajifunze hilo. Milan mpaka sasa imeambulia alama nne katika mechi nne za Serie A walizocheza lakini Allegri bado ana imani na kikosi chake kwamba kinaweza kubadilika na kufanya vyema katika siku zijazo.
Mario Balotelli akichonga penati ambapo kipa aliudaka mkwaju huo.

Pepe Reina akidaka mkwaju wa Balotelli

Gonzalo Higuain akifunga bao
Miguel Britos akiipatia bao la pili Napoli

Acrobatics: Balotelli
No comments:
Post a Comment