Sunderland wamemtimua Meneja wao Paolo
Di Canio baada ya mwanzo mbovu kwenye Ligi Kuu England ambapo Timu hiyo
imejikuta ipo mkiani kwenye Msimamo wa Ligi hiyo.
Tangu ateuliwe kuwa Meneja wa Sunderland
Mwezi Machi, Di Canio, mwenye Miaka 45, ameshinda Mechi 3 tu kati ya 13
alizosimamia na Msimu huu ameambua Pointi 1 tu katika Mechi za Ligi 5.
Klabu ya Sunderland imetoa tamko kuwa
mrithi wa Di Canio atatangazwa hivi karibuni na kwa sasa Timu hiyo
itakuwa chini ya Kocha Kevin Ball.
Mechi
ya kwanza chini ya Kocha Kevin Ball itakuwa ni Jumanne watakapocheza
Nyumbani Stadium of Light na Peterborough United kwenye Raundi ya Tatu
ya Capital One Cup.
Baada ya Mechi hiyo, Sunderland watakuwa
Wenyeji kwa Liverpool Jumapili ijayo, kisha kucheza na Manchester
United Oktoba 5 na kufuatia Dabi ya eneo la Wear-Tyne dhidi ya Newcastle
hapo Oktoba 27.
Mwezi Machi Mwaka huu, Di Canio alitinga
Sunderland kuchukua nafasi ya Martin O'Neill, aliefukuzwa na
akakaribishwa na madai kuwa yeye anasapoti Mafashisti.
Meneja huyo kutoka Italy mwenye vituko
amekuwa mwepesi kuwaponda Wachezaji wake waziwazi Magazetini na hili
limeleta mkwaruzo ndani ya Timu.
Msimu huu, Di Canio alianza kwa kipigo
cha Nyumbani na Fulham, Sare na Southampton na kisha vipigo toka kwa
Crystal Palace, Arsenal na hivi Juzi West Brom.
Mbali ya kusaini Wachezaji 14 kwa ajili ya Msimu huu mpya, Di Canio pia aliwauza Wachezaji mahiri
Kama Kipa Simon Mignolet kwa Liverpool
na Stephane Sessegnon kwa West Brom ambae hivi Juzi katika Mechi yake
kwanza tu na West Brom alifunga Bao walipoicharaza Sunderland 3-0.
Sunderland sasa inasaka Meneja mpya wa 6 katika kipindi cha chini ya Miaka mitano.
ANGALIA MITANANGE YOTE ALIYOSIMAMIA SUNDERLAND MPAKA ANAFUKUZWA.
2012-13
April 7 - Chelsea 2 Sunderland 1 (L)Apr 14 - Newcastle 0 Sunderland 3 (W)
Apr 20 - Sunderland 1 Everton 0 (W)
Apr 29 - Aston Villa 6 Sunderland 1 (L)
May 6 - Sunderland 1 Stoke 1 (D)
May 12 - Sunderland 1 Southampton 1 (D)
May 19 - Tottenham 1 Sunderland 0 (L)
2013-14
August 17 - Sunderland 0 Fulham 1 (L)Aug 24 - Southampton 1 Sunderland 1 (D)Aug 27 - Sunderland 4 MK Dons 2 [Capital One Cup] (W)
Aug 31 - Crystal Palace 3 Sunderland 1 (L)September 14 - Sunderland 1 Arsenal 3 (L)
Sep 21 - West Brom 3 Sunderland 0 (L)
KUHUSU DI CANIO
-KUZALIWA: Rome, 9 Julai 1968
-KLABU ALIZOCHEZA: Lazio, Juventus, Napoli, AC Milan, Cisco Roma, Celtic, Sheffield Wednesday, West Ham, Charlton
-FAINI: £10,000 Mwaka 1998 kwa kumsukuma na kumwangusha Refa Paul Alcock baada ya kutolewa katika Mechi dhidi ya Arsenal
-TUZO YAUCHEZAJI WA HAKI: Mwaka 2001 kwa kudaka Mpira badala ya kufunga ili Kipa wa Everton Paul Gerrard apate Huduma ya Kwanza baada kuumia.
-APONDWA: Mwaka 2005 kwa kutoa Saluti ya Kifashisti kwenye Gemu na Lazio.
-ATEULIWA: Bosi wa Swindon Mei 2011 na kuwapandisha LIGI 1 Mwaka mmoja baadae
-AJIUZULU: Kama Bosi wa Swindon Februari 2013
-AMBADILI: Martin O'Neill kama Meneja wa Sunderland Machi2013 na kuinusuru kushushwa Daraja toka Ligi Kuu England.
-ATIMULIWA: Sunderland baada Mechi 5 za Ligi ambazo amefungwa 4 kati ya hizo na Sare moja.
No comments:
Post a Comment