
Rafael Nadal akishangilia kwa kubeba kombe baada ya kumgaragaza t Novak Djokovic kwenye set nne
MCHEZAJI nyota wa tenisi anayeshika namba mbili katika orodha za ubora duniani, Rafael Nadal amefanikiwa kutawadhwa bingwa mpya wa michuano ya wazi ya Marekani baada ya kumfunga Novak Djokovic wa Serbia katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Arthur Ashe jijini New York. Nadal ambaye ni raia wa Hispania alifanikiwa kumtuliza Djokovic ambaye anashika namba moja katika orodha hizo kwa seti 3-1 zenye alama za 6-2 3-6 6-4 6-1 katika mchezo uliotumia saa tatu na dakika 21. Nyota huyo sasa ameshinda mataji 13 ya Grand Slam na kuingia katika orodha ya wachezaji waliowahi kushinda mataji mengi zaidi akiwemo Pete Sampras na Roger Federer anayeongoza orodha hiyo kwa kushinda mataji 17 ya Grand Slam. Ushindi huo sasa utamuwezesha Nadal kurejea namba moja katika orodha hizo akichukua nafasi ya Djokovic ambaye atashuka mpaka namba mbili.
Djokovic(kulia) hoi!! baada ya kupewa kichapo cha aina yake na Nadal na hapa ni baada ya kupewa kifuta machozi baada ya mchezo kuisha na kumtangaza Nadal kama mshindi mpya 2013.

Djokovic alijitahidi mpaka mwisho lakini bahati haikuwa yake tena zamu hii.
Nadal akionekana kuwa mwenye nguvu na bidii sana na kufanikiwa kumwangusha Djokovic
Djokovic kazini
David Beckham nae kama kawaida alikuwepo tena humo uwanjani kushuhudia kipute hicho cha aina yake!

Beckham akipeana jambo na Kevin Spacey huku wakitokelezea kwenye picha.
Djokovic raundi ya nne alionekana kama hayumo tena hewani!!! Na hapa alikuwa na mawazo mengi sana!
Nadal aliibuka shujaa kwa kumshinda Djokovic
Staa Leonardo DiCaprio nae alikuwepo mahala hapo!!
Jessica Alba na Amanda Seyfried hao wakichungulia mchezo huo mkali

Mwanamuziki Justin Timberlake akicheki fainali hizo nae
Mcheza filamu Sean Connery na Alec Baldwin nao walikuwa moja ya mashabiki uwanjani hapo

Mwisho wa ubaya:mshindi na aliyeshindwa wakiponezana hapa!!
No comments:
Post a Comment