BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 24, 2013

RATIBA CAPITAL ONE CUP: RAUNDI YA 3 DIMBANI JUMANNE & JUMATANO. SUAREZ KUCHEZA MTANANGE HUO BAADA YA KUMALIZA KIFUNGO CHAKE CHA MECHI 10.


MECHI za Raundi ya Tatu ya CAPITAL ONE CUP zitachezwa Jumanne na Jumatano huku Klabu ambazo zinashiriki michuano ya UEFA Ulaya zikianza kushiriki.
Mabingwa Watetezi Swansea City wamepangiwa kwenda kucheza Ugenini na Timu ya Daraja la Championship Birmingham.
Mechi zitakazohusisha Timu za Ligi Kuu pekee ni zile za Aston Villa v Tottenham, West Brom v Arsenal, West Ham v Cardiff na Everton v Fulham.
Jumatano ndio ‘Bigi Mechi’ huko Old Trafford ambapo Manchester United watawavaa Mahasimu wao wakuu Liverpool na hii Mechi inamvuto mkubwa hasa kwa vile Jumapili huko Etihad Man United walichapwa Bao 4-1 kwenye Ligi na Mahasimu wao wengine Man City na Wadau wanataka kujua kulikoni.
Jumatano huenda ikawa ndio Mechi ya kwanza ya Straika wa Liverpool Luis Suarez baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi 10 kwa kumng’ata Branisla Ivanovic wa Chelsea kwenye Mechi.
CAPITAL ONE CUP
RATIBA
Jumanne Septemba 24
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Sunderland v Peterborough
West Ham v Cardiff
Man City v Wigan
Burnley v Nottingham Forest
Southampton v Bristol City
Swindon v Chelsea
Watford v Norwich
Aston Villa v Tottenham
Hull v Huddersfield
Leicester v Derby
[Saa 4 Usiku]
Fulham v Everton
Jumatano Septemba 25
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Swansea
Manchester United v Liverpool
Newcastle v Leeds
Tranmere v Stoke
[Saa 4 Usiku]
West Brom v Arsenal

No comments:

Post a Comment