BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 24, 2013

ROBIN VAN PERSIE KUWAVAA LIVERPOOL OLD TRAFFORD KWENYE RAUNDI YA TATU YA CAPITAL ONE CUP.

David Moyes amethibitisha kuwa Robin van Persie hakuumia sana kiasi cha kumfanya aikose pia Mechi ya Manchester United ya Jumatano na Liverpool Uwanjani Old Trafford ambayo ni ya Raundi ya Tatu ya Capital One Cup.
Jumapili, Van Persie hakucheza kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huko Etihad walipofungwa 4-1 na Man City.
Moyes alisema: “Tunafikiri yuko sawa. Tutampa kila nafasi. Hakuumia sana.”
Moyes alibainisha kuwa Staa huyo alikuwa akisikia maumivu kidogo kwenye Nyonga na ili kumlinda asijiumize zaidi waliamua kumpumzisha kwenye Mechi na Man City.
Lakini, baada ya Jumapili kufungwa na Mahasimu wao Man City, Mechi hii na Mahasimu wao wakubwa zaidi na wa Kihistoria, Liverpool, sasa imekuwa ya kusaka ushindi wa kufa na kupona na upo umuhimu kwa Man United kubahatisha kwa kumuanzisha Mfungaji wao Bora kabisa.

No comments:

Post a Comment