
Serena Williams wa Marekani akibeba kombe lake baada ya kumfunga Victoria Azarenka wa Belarus kwenye 2013 US Open jana jumapili.

Serena Williams akipozi mbele ya wapiga picha kupigwa picha baada ya kumshinda kete Victoria Azarenka
Mchezaji Tenesi nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams amedai kuwa angeshindwa kutwaa taji la US Open kwa mwaka huu ungekuwa ni mwaka wake mbaya zaidi kwenye historia ya mchezo huo.
Serena ambaye alikuwa akitetea taji lake, ameibuka na ushindi baada ya kumfunga Victoria Azarenka kwa seti mbili moja kwa matokeo ya 7-5, 6-7 na 6-1 kwenye mchezo ambao ulilazimika kuchezwa kwa zaidi ya saa mbili.
Serena Williams amefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa kushinda taji la tano la michuano ya wazi ya Marekani baada ya kumfunga Victoria Azarenka wa Belarus katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini New York. Williams ambaye anashika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake alifanikiwa kumgaragaza kwa Azarenka anayeshika namba mbili kwa 7-5 6-7 6-1.
Sasa Williams raia wa Marekani ameshinda mataji 17 ya Grand Slams na kumpaisha mpaka katika nafasi ya tano katika wachezaji ambao wamewahi kushinda mataji mengi zaidi ya Grand Slams katika historia ya mchezo huo.
Akihojiwa mara baada mchezo huo Williams alimsifu Azarenka kwa kucheza vyema hivyo kuufanya mchezo kuwa mgumu mpaka katika seti ya mwisho. Azarenka mwenye umri wa miaka 24 amemfunga Williams mara mbili kwa mwaka huu, huku mara ya mwisho ikiwa katika fainali ya michuano ya Cincinnati ambayo huchezwa kabla ya michuano ya US Open.
Azarenka kazini jana akipigana vikali na Serena

Azarenka

Dada wa Serena, Venus na mama Oracene wakimcheki
Boris Beckerakichukua picha kwa simu
Serena hakuwa na msimu mzuri kwa mwaka huu baada ya kupoteza pia taji la Australian Open baada ya kutolewa kwenye hatua ya robo fainali na mwanadada Sloane Stephens na kisha kutuowa nje kwenye michuano ya Wimbledon kwa kfungwa kwenye hatua ya nne na Lisick Sabine.
Leo ni fainali kwa upande wa wanaume ambapo Rafael Nadal atakutana na mchezaji nambari moja kwa mchezo huo upande wa wanaume, Novak Djokovic.
No comments:
Post a Comment