Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini
Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo
Mara baada ya zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.
Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR_MAGEUZI, James Mbatia akisahangaa kuona mapambano kati ya wabunge wa CHADEMA na Polisi Bungeni
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo. hata hivyo Microphone hiyo iling'oka na polisi wakafaikiwa kumtoa nje
Microphone hiyo iling'oka na polisi wakafanikiwa kumtoa nje
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akitolewa na Askari Polisi nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya hivyo na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai
Mbunge wa Mbeya Mjini akizuiwa na wabunge wa CHADEMA ili asipambane na polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo
Kwa hisani ya MUHIDIN MICHUZI
No comments:
Post a Comment