L'Equipe limechukua idadi ya Wapenzi ya kila Mwanamichezo maarufu kwenye Kurasa zao za Mtandao wa Facebook na kuangalia Mwanamichezo yupi kapewa ‘Gonga za Sapoti’, yaani ‘LIKEs’ nyingi, na katika 10 Bora Duniani Wanasoka wako 6, Mpira wa Kikapu watatu na Tenisi mmoja huku Mwanasoka Cristiano Ronaldo akiwa Nambari Wani kwa Likes 60,274,869 akifuatiwa na Lionel Messi mwenye 48,000,104.
TAKWIMU:
JINA | MCHEZO | FACEBOOK LIKES |
C. Ronaldo | Soka | 60,274,869 |
Lionel Messi | Soka | 48,000,104 |
David Beckham | Soka | 29,150,690 |
Michael Jordan | MPIRA KIKAPU | 23,817,809 |
Kaka | Soka | 23,477,568 |
Kobe Bryant | MPIRA KIKAPU | 16,693,216 |
LeBron James | MPIRA KIKAPU | 14,802,829 |
Andres Iniesta | Soka | 14,357,223 |
Neymar | Soka | 13,388,531 |
Roger Federer | TENISI | 13,289,792 |
Listi hiyo ya 10 Bora imewabwaga Majina
makubwa ya Wanamichezo maarufu kama vile Usain Bolt, Michael Phelps,
Sebastian Vettel, Sachin Tendulkar, Tiger Woods, Floyd Mayweather na
Rafa Nadal.

Mchezaji ambae Juzi alivunja Rekodi ya kuwa mwenye Bei ghali Duniani, Gareth Bale, yupo Nafasi za chini akiwa na ‘Likes’ chini ya Milioni 5 kwenye Ukurasa wake wa Facebook.
Mchezaji ambae Juzi alivunja Rekodi ya kuwa mwenye Bei ghali Duniani, Gareth Bale, yupo Nafasi za chini akiwa na ‘Likes’ chini ya Milioni 5 kwenye Ukurasa wake wa Facebook.
No comments:
Post a Comment