BUKOBA SPORTS

Friday, October 11, 2013

DEREVA MASHUHURI WA F1 MARIA DE VILLOTA AFARIKI DUNIA.

Maria de VillotaMarie De Villota
Dereva mashuhuri mwanamke wa mashindano ya langalanga Formula 1 Maria De Villota amepatikana amefariki ndani ya chumba cha hoteli moja mjini Seville, Hispania.
Msemaji wa polisi alisema."Tunachukulia kilikua kifo cha kawaida,lakini hatuwezi kuthibitisha chochote na uchunguzi utafanywa kuhusu kifo chake"
De Villota, mwenye umri wa miaka 33,alikua dereva wa akiba wa langalanga. Alipofuka jicho lake la kulia katika ajali ya mwezi wa Julai mwaka jana alipokua akifanya mazoezi na timu ya Marussia.
Alipata majeraha mabaya kichwani na usoni baada ya kugongana na lorry katika jimbo la Cambridgeshire, Uingereza lakini aliruhusiwa kuanza tena kuendesha gari.

Iliarifiwa De Villota, binti wa dereva wa zamani wa mashindano ya Formula 1, Emilio De Villota,alikwenda Seville kuzindua kitabu kuhusu maisha yake.
Timu na madereva wa langalanga wameelezea kushtushwa kwao na msiba huo.
Jenson Button wa Uingereza amesema. "inasikitisha sana. Msichana huyu amekumbwa na masaibu mengi sana, kupita yale yanayowakumba watu wengi duniani. Ni habari zilizotushtuwa timu nzima na jamii nzima ya mbio za langalanga."
"tulimuona mwaka huu mjini Barcelona.Tukifanya kazi kwa wakfu wa kuwasaidia watoto na alikua wa kwanza kujitolea na kuwashawishi madereva wengi kujiunga nasi.Alikua akichangia mengi kwa jamii ."Incident: An ambulance leaves the Congresos Hotel in Seville Incident: An ambulance leaves the Congresos Hotel in Seville
Tragedy: Maria De Villota was the guest of honour at the Spanish Grand Prix earlier this season
Maria De Villota was the guest of honour at the Spanish Grand Prix earlier this season.

KUHUSU MARIA DE VILLOTA:
1980: Born January 13, in Madrid, Spain
1996-2000: Competes in various forms of karting.
2002-06: Drives in the Spanish F3 championship, with a best result of third in Jarama.
In 2004 takes part in the Daytona 24 Hours, finishing ninth in the GT class in a Ferrari Modena.
2007: Competes in the German Touring Car Championship and WTCC with Chevrolet.
2008: Claims a best finish of seventh in the Formula 3000 Euroseries.
2009-10: Drives for Atletico Madrid in the now defunct Superleague Formula, with a high of fourth at the Nurburgring.
2011: Has a test with Lotus Renault GP at the Paul Ricard Circuit in August.
2012March - signs for Marussia as test driver.
June - Becomes one of the four founding figures of the Women & Motorsport Commission designed to increase the presence of women in motorsport.
July - Loses her right eye in a freak accident at Duxford Aerodrome while straight-line testing with Marussia. Spends a month in hospital.
2013October 11 - Is found dead in a hotel room in Seville.

No comments:

Post a Comment