Sunday, October 6, 2013
ENGLISH PREMIER LEAGUE:WEST BROM 1 v ARSENAL 1, GUNNERS HAO KILELENI USIKU HUU WALAZIMISHA SARE NA WEST BROM!, IKISAWAZISHIWA NA "MCHOMAJI" WILSHERE!
Timu ya Gunnes imelazika kutoka sare na timu ya West Bromwich Albion kwa kufungana bao moja moja, West Bromwich ndiyo walianza kuziona nyavu za Arsenal kupitia mchezaji wao Claudio Yacob dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza dakika ya 42. Wao Gunners wamesawazisha kipindi cha pili dakika ya 63 Jack Wilshere anaisawazishia bao Gunners na kufanya 1-1. Sare hii inawapandisha Arsenal nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 16 sawa na Liverpool ambao pia wanapointi hizo hizo wakitofautiana ubora wa goli la nyumbani na ugenini.Kipindi cha kwanza dakika ya 42 mchezaji wa West Bromwich Claudio Yacob akaifungia bao kwa kichwa safi kwa kudundisha mpira ambao umemshinda mchezaji kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny. Mchezaji mpya West Bromwich Albion Nicolas Anelka akichuana na Mikel Arteta wa Arsenal katika kipindi cha kwanza
Claudio Yacob na Mathieu Flamini wakikimbiza mpira.
Hakuna kufanya makosa: Jack Wilshere akifunga bao kusawazisha hapa!
Aaron Ramsey akigombea mpira na Liam Ridgewell
Mesut Ozil akionesha kiwango tena leo hii..
Mchezaji wa West Brom Claudio Yacobakifunga bao dakika ya 42 muda mchache kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza
Yacob akipongezwa na wenzie Nicolas Anelka na Stephane Sessegnon
Arsenal baada ya kufungwa !!!
Mchezaji wa Gunners Laurent Koscielny akeindesha!!
Jack Wilshereakifunga bao lake hapa kipindi cha pili
Olivier Giroudakishangilia bao la Wilshere baada ya kusawazisha kipindi cha pili.
Kieran Gibbs akizuia mpira hapa katika kipindi cha pili cha mchezo wao wakiwa ugenini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment