Thursday, October 3, 2013

EUROPA LEAGUE: ANZHI MAKHACHKALA 0 v TOTTENHAM 2, DEFOE NA NACER CHADLI WAIPATIA USHINDI SPURS!!

Tottenham wakiwa ugenini huko Urusi kucheza na Anzhi Makhachkala, Spurs wameanza kuifunga Anzhi Makhachkala katika dakika ya 34 Jermain Defoe akifunga bao hilo na bao la pili likafungwa na mchezaji wao Nacer Chadli baada ya dakika 5 kupita katika dakika ya 39 kipindi cha kwanza.
Odil Ahmedov akichomoa mpira kwa Ezekiel Fryers wa Spurs Mchezaji Jermain Defoe wa Tottenham Hotspur akifunga bao la kwanza hapa dakika ya 34

Mchezaji wa Tottenham Lewis Holtby akichuana na Abdul Raza Abdul Razak na  Moussa Dembele kwenye patashika..usiku huu. Ewerton akimzuia Erik Lamela wa Spurs hapa
Kipindi cha pili pamoja na Anzhi Makhachkala kuja kwa kasi dakika mwazoni mwa kipindi cha pili hawakuweza kuona lango la Spurs na wakaishia kuzungushwa na Tottenham Hotspur na dakika 90 za mtanange huo zikaisha kwa Spurs wakiwa na ushindi muhimu wa Alama tatu katika raundi hii ya Mechi za Pili za Makundi Europa Ligi.

EUROPA LIGI
RATIBA/MATOKEO
Alhamisi Oktoba 3

19:00 FC Anzhi
0 v 2
Tottenham Hotspur
19:00 FC Rubin Kazan
4 v 0
SV Zulte Waregem
19:00 FC Kuban
0 v 2
Valencia
19:00 Shakhter Karagandy
2 v 2
Maccabi Haifa
MITANANGE MINGINE YA EUROPA IPO INAENDELEA...

No comments:

Post a Comment