Tuesday, October 8, 2013

FRANCIS CHEKA CHEKA AITWA MUHEZA KUHAMASISHA NGUMI


BINGWA wa dunia wa kanda wa WBF, Fransic Cheka amealikwa wialayani Muheza mkoani Tanga kwa lengo la kutoa hamasa kwa mchezo wa ngumi wilayani hapo.

Kocha wa Ngumu wa Muheza, Charles Muhiru amesema wamemualika Cheka wilayani kwao ili kutoa hamasa kwa mabondia wao ambao nao wana kiu ya kufikia mafanikio ya Cheka.
Muhiru alisema kuwa Cheka atafika Muheza siku ya sikukuu ya pili ya Idd Alhaji na kushuhudia mapambano ya ngumi ya mabondia wa wilayani humo ambayo yatafanyika kwenye Viwanja vya Jitegemee.
Kocha huyo pia aliombva kuungwa mkono na wadau wa mchezo huo kwa lengo la kutoa sapoti kubwa ili kufanikisha ziara hiyo sambamba na mchezo huo kwa ujumla ili kuwawezesha vijanja wanaoingia katika mchezo huo kupata mafanikio na kuliletea taifa sifa kama ilivyokuwa kwa Cheka.

No comments:

Post a Comment