Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania kiwanda cha Arusha wakicheza fussball katika hafla ndogo ya kutambulisha kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi hao kabla ya uzinduzi mkubwa utakaofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kampeni hiyo itawashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kwa muda wa miezi miwili kupitia matukio mbalimbali.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kiwanda cha Arusha, Idrisa Athumani akishiriki katika shindano la kupiga danadana katika hafla ndogo ya kutambulisha kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi hao kabla ya uzinduzi mkubwa utakaofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kampeni hiyo itawashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kwa muda wa miezi miwili kupitia matukio mbalimbali. (Picha: Mpiga Picha Wetu, Arusha)
No comments:
Post a Comment