BUKOBA SPORTS

Sunday, October 13, 2013

KOMBE LA DUNIA AFRICA: ETHIOPIA 1 v NIGERIA 2, EMMANUEL CHINENYE EMENIKE AIONESHA NIGERIA MLANGO WA BRAZIL!! ATUPIA 2 UGENINI!

Mabingwa wa Afrika, Nigeria leo wamewachapa Ethiopia kwao huko Addis Ababa bao 2-1. Ethiopia wakitandaza kandanda safi nyumbani na wakipata mashabiki wa kutosha wao ndio walianza kuifunga Nigeria dakika ya 57 Baada ya kupigwa shuti kali la Mengitsu Assefa na kipa wa Nigeria V. Roar of delight: Emmanuel Emenike (centre) celebrates after converting the winner from the spotEnyeama kudakia mpira ndani ya goli, Baadae Nigeria walichangamka na kusawazisha bao hilo kipindi cha pili. Baada ya kufanya mabadiliko haraka na dakika ya 67 Mshambulia anayekipiga katika soka la kulipwa katika Klabu ya Fenerbahçe Emmanue Chinenye Emenike akawachambua wachezaji wa Ethiopia na kuachia mkwaju uliozama kwa kupanguliwa na kipa wa Ethiopia ndani ya lango lao, Dakika ya lala salama dakika ya 90 Nigeria walipata penati na mchezaji huyo huyo hatari Emenike akapiga penati hiyo na kufanikisha ushindi Ugenini wa bao 2-1 dhidi ya Ethiopia. Mwanzoni Ethiopia walipata bao baada ya Mchezaji wa Nigeria kuuokolea ndani lakini Refa na Msaidizi wake hawakuweza kuliona bao hilo na kisha kupeta.Emenike akifunga penati hapa dakika ya 90 Dispatched: Emenike tucked his penalty home coolly, leaving the keeper with no chanceEmenike kulia akishangilia bao hilo la pili

USO KWA USO KUKUTANA
. Nigeria 3 Vs Ethiopia 0, 1982 Nations cup finals.
· Ethiopia 0 Vs Nigeria 0, 1993 Friendly match, Addis Ababa
· Ethiopia 1 Vs Nigeria 0, 1994 Nation cup 1st leg qualifier, Addis Ababa
· Nigeria 6 Vs Ethiopia 0, 1994 Nation cup 2nd leg qualifier, Lagos
· Ethiopia 2 Vs Nigeria 2, 2012 AFCON 1st leg qualifier, Addis Ababa
· Nigeria 4 Vs Ethiopia 0, 2012 AFCON 2nd leg qualifier, Abuja
· Nigeria 2 Vs Ethiopia 0, 2013 AFCON finals, South Africa
*Na Leo sasa ni 2-1

RATIBA/MATOKEO
Mechi za Kwanza:

Jumapili Oktoba 13
Ethiopia 1 v Nigeria 2 (E. Emenike)
20:00 Tunisia v Cameroon


RATIBA:
Mechi za Kwanza:
Jumanne Oktoba 15

19:00 Ghana v Egypt

Marudiano:
Jumamosi Novemba 16

18:00 Nigeria v Ethiopia
22:00 Senegal v Ivory Coast
Jumapili Novemba 17
17:30 Cameroon v Tunisia
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana
21:15 Algeria v Burkina Faso

No comments:

Post a Comment