MABAO matatu aliyofunga mshambuliaji wa kimataifa Uholanzi Robin van Persie katika ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Hungary wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia umemfanya kuwa mshambuliaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika nchi yake. Van Persie alifikisha mabao 41 katika mechi 80 alizocheza katika timu ya taifa na kuizidi rekodi iliyowekwa na Patrik Kluivert katika mechi hiyo iliyopigwa jana usiku. an Persie ambaye anacheza katika klabu ya Manchester United alifunga bao la kuongoza kwa timu yake katika dakika ya 15 kabla ya kuifikia rekodi hiyo ya mabao ya taifa kwa kufunga bao lingine kabla ya mapumziko. Nyota huyo aliongeza bao lingine katika dakika 52 na kufanya idadi ya mabao aliyoifungia timu ya taifa kufikia 41 na kumpita Kluivert aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kufunga mabao 40.
No comments:
Post a Comment