Eto’o ambaye alistaafu kuichezea timu hiyo lakini alirudi baada ya kuombwa na rais wa nchi hiyo, lakini pamoja na kuwa uwanjani timu yake ilimaliza mchezo huo uliochezwa jijini Tunis kwa suluhu.
Miamba hiyo inatarajia kurudiana tena Novemba 17 jijini Yaunde na matokeo ya mchezo huo ndiyo yatatoa nani anaweza kutinga nchini Brazil kushiriki fainali hizo kati yao.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani katika dakika zote 90, Tunisia walikuwa wakiliandama lango la wapinzani wao lakini shukrani kwa kipa wa zamani wa Liverpool, Charles Itandje ambaye aliisaidia Camerron kuokoa michomo mingi langoni kwake.
Timu hizo zote zimeshacheza kombe la dunia mara tisa hivyo wanawania nafasi ya 10 kucheza michuano hiyo mikubwa duniani, hivyo ushindani katika mchezo wa marudiano utakuwa mkubwa zaidi ya jana usiku.
AFRIKA Raundi ya Mwisho ya Mtoano
Mechi za Kwanza:
MATOKEO/MATOKEO
Jumapili Oktoba 13
Ethiopia 1 Nigeria 2
Tunisia 0 Cameroon 0
Jumamosi Oktoba 12
Burkina Faso 3 Algeria 2
Ivory Coast 3 Senegal 1
RATIBA:
Jumanne Oktoba 15
19:00 Ghana v Egypt
No comments:
Post a Comment