BUKOBA SPORTS

Sunday, October 6, 2013

MISS TOURIST TANZANIA 2013 AONDOKA NCHINI KWENDA EQUATORIAL GUINNEA KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA


Miss Tourist Tanzania 2013 Hadija Said akiondoka uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere

Rais wa Miss Utalii Chipungahelo akimkabidhi cd pamoja na vipeperushi vya hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuitangaza hifadhi hiyo akiwa huko Equtorial Guinnea

Miss Tourist 2013 Hadija Said (kushoto) akiwa pamoja na mrembo mwenzake Theresia Kimolo aliymsindikiza

MREMBO wa Utalii Tanzania 2013 (Miss Tourist Tanzania 2013) Hadija Said ameondoka nchini leo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya urembo ya dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Equatorial Guinnea
Mashindano hayo ya Miss Utalii yanatarajiwa kufanyika Otoba 12, mwaka huu kwenye mji wa Malabo na jumla ya nchi 126 zinatarajiwa kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, mrembo Hadija Saidi alisema anaamini anakwenda kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema kama warembo wenzake waliotangulia kushiriki katika fainali hizo za dunia.
“Naamini nakwenda huku na nitarudi na taji kama walivyofanya warembo walionitangulia”, alijigamba Hadija.
Pia aliishukuru mamalaka ya hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kwa kudhamini safari yake na anaamini anakwenda kuitangaza vyema hifadhi hiyo ambayo ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia akiwemo Nyati mweupe aliyeonekana hivi karibuni katika hifadhi hiyo.
Mashindano ya Miss Utalii yalianza nchini mwaka 2004 hadi 2007 na yalisimama kwa miaka kwa miaka mitano hadi yalipokuja kufanyika tena mwaka huu mkoani Tanga na mara zote kila mwakilishi anayewakilisha nchini anarudi na taji.

No comments:

Post a Comment