Miss Ufilipino, Megan Young, juzi aliibuka mshindi wa Miss World 2013 kwenye fainali zilizofanyika katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia ambako kulikuwa na ulinzi mkali.
Megan Young, Miss World 2013
“Naahidi kuwa Miss World bora zaidi,” Young mwenye miaka 23, alisema baada ya kushinda fainali hizo za 63 wakati ambapo Wafilipino kibao waliokuwa wamesafari kwenda kushuhudia fainali hizo wakisherehekea kwa kurukaruka na kupeperusha bendera ya nchi yao kwa furaha.
Licha ya kuwepo vitisho kutoka kwa kundi la Islamic Defenders Front kuwa lingeshambulia shindano hilo, polisi walisema hakuna maandamano yaliyofanyika jana. Warembo 127 walishiriki kwenye shindano hilo.
Kutoka Kushoto: Miss Ufaransa, Marine Lorphelin, 20, aliyekamata nafasi ya pili, Megan Young na Miss Ghana, Carranzar Naa Okailey Shooter, 22, aliyekamata nafasi ya tatu
Mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, akiwa amemkumbatia mrithi wake
Megan ameshaigiza filamu zaidi ya 10 nchini Ufilipino zikiwemo The Reunion na Bang Bang Alley
Young, aliyemrithi mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, alizaliwa nchini Marekani. Alipokuwa na miaka 10 alirudi kwao Ufilipino ambako ameonekana kwenye filamu na kufanya kazi kwenye TV.
Zaidi ya polisi 700 walimwagwa kuhakikisha usalama wakati wa fainali hizo
No comments:
Post a Comment