Na Mwandishi Wetu
REDD’S Miss Tanzania 2012/2013, Brigitte Alfred ambaye pia alifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika shindano la Beauty With a Purpose wakati wa kuwania taji la dunia (Miss World) mwaka huu, amerejea nchini na kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono kwa kipindi chote alichokuwa akishikilia taji hilo.
Brigitte alifanikiwa kushika nafasi hiyo katika shindano hilo, ambalo lilishirikisha warembo zaidi ya 190 kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambalo lilikuwa mahususi kwa warembo kuonyesha kazi walizofanya kwa jamii katika nchi wanayotoka.
Mrembo huyo alionyesha jinsi alivyosaidia kwa kiasi kikubwa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalumu hasa wale wenye ulemavu wa ngozi.
Akizungumzia kuhusu shindano la Miss World alisema, lilikuwa na changamoto nyingi na anaamini ni lazima Watanzania wajivunie mafanikio ambayo yamefikiwa mpaka sasa katika mashindano hayo ya dunia.
Mafanikio makubwa zaidi ambayo Tanzania iliwahi kuyapata ni pale Nancy Sumari alipofanikiwa kutwaa taji la Miss World Africa katika mashindano yaliyofanyika mwaka 2005.
Kuhusu kipindi chote alichokuwa akishikilia taji la Redds Miss Tanzania alisema, alipata ushirikiano mkubwa na akatoa shukrani kwa jamii kumuunga mkono kwa kipindi chote hicho.“Napenda kutoa shukrani za dhati kwa Kamati ya Redd’s Miss Tanzania, wazazi wangu, vyombo vya habari, Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa kuniunga mkono kwa kipindi chote hicho.
“Kusema kweli sina cha kuwalipa na naahidi nitaendelea kushirikiana na kamati hii katika kuhakikisha Tanzania inafanya vyema zaidi katika mashindano ya dunia siku za baadaye,” alisema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Redd’s Miss Tanzania alisema, wanajivunia kwa kiasi kikubwa mafanikio yaliyofikiwa na Brigitte katika mashindano hayo.
“Kwetu tunachukua fursa hii kuyaomba makampuni au taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini mashindano haya kwani ni muhimu zaidi kwa ustawi wa Taifa,” alisema.
Taji la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Happiness Watimanywa ambaye alifanikiwa kulitwaa hivi karibuni.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:
Post a Comment