Heshima hii aliyopewa Sir Alex Ferguson ni kwa kutambua mafanikio yake akiwa na Klabu ya Manchester United kati ya Mwaka 1986 hadi 2013 kipindi ambacho alitwaa Mataji 38.
Sir Alex anafuata nyayo za Lejendari mwingine wa Man United, Sir Matt Busby, ambae Mwaka 1993 Mtaa uitwao Warwick Road North ulibadilishwa Jina na kuitwa Sir Matt Busby Way.
Ferguson, mwenye Miaka 71, tayari anazo heshima nyingine ikiwa ni pamoja na Jukwaa moja la Uwanja wa Old Trafford kuitwa Sir Alex Ferguson Stand na pia Sanamun yake ya Shaba kusimikwa nje ya Uwanja huo.
Huko kwao Scotland, Sir Alex Ferguson ameshapewa ‘Uhuru wa Jiji la Glasgow.’
Hivi sasa, Ferguson ni Mkurugenzi kwenye Klabu ya Man United.
Sir Alex Ferguson receives the Freedom of the Borough of Trafford from Mayor Dylan Butt (left) on Monday. Also pictured are Trafford Council leader Matt Colledge (second left), chief executive Theresa Grant (second right) and Ferguson's wife Cathy (right).
Ferguson alishinda 38 Old Trafford, ikiwa pamoja na la mara ya 13 Premier League
Ferguson pia aliwawezesha Man United kushinda kombe la Champions League mwaka 2008
Enzi hizo: Ferguson akiwa amebeba kombe la FA baada ya United kuwafunga Millwall 3-0 kwenye Uwanja a Cardiff mwaka 2004 - akiwa ameshinda mara 5
LIGI KUU: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013
FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
UEFA CHAMPIONZ LIGI: 1999, 2008
UEFA KOMBE LA WASHINDI: 1991
FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
UEFA SUPER CUP: 1992
INTER-CONTINENTAL CUP: 1999
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
No comments:
Post a Comment