Hakunaga: Historia ndefu ya 99 tunairudisha tena hapa ....Winston Reid akishangilia kwa furaha kubwa na kupongezwa!!
Ravel Morrisonakitupia kuwaua zaidi Spurs na wakiwa nyumbani kwao White Hart Lane
Mashabiki wa West Ham United wakiwazodoa mashabiki wa Spurs kwenye uwanja wao White Hart Lane
Kevin Nolan akifurahia bao kwa West Ham
TOTTENHAM 0 v WEST HAM 3 BAO 3 za Kipindi cha Pili zimewapa West Ham ushindi wao wa kwanza Uwanjani White Hart Lane tangu Mwaka 1999 walipoitwanga Tottenham 3-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Ushindi huu pia umewatoa West Ham toka Timu 3 za Mkiani na kupanda hadi Nafasi ya 13.
Winston Reid ndie alieipa West Ham Bao la Kwanza kwenye Dakika ya 66, Vaz Te kupiga Bao la Pili Dakika ya 73 na Chipukizi wa Miaka 20 alieanzia Soka lake Man United, Ravel Morrison, alifunga Bao zuri la 3 katika Dakika ya 79 baada kuchukua Mpira toka Nusu yao ya Uwanja na kuwatambuka Mabeki kadhaa wa Spurs na kufunga kifundi.
James Tomkins akiachia mkwaju hapa..
James Corden na Michael McIntyre wakiangalia mtanange wakiwa wamesimama kwenye uwanja wa White Hart Lane
Michael Dawson kwenye mbio, akikabana na Ricardo Vaz Te
Mashabiki wakiwa wamejikinga jua usoni na vipigo vikiendelea kwenye uwanja wa White Hart Lane, Spurs wakitupiwa tatu kipindi cha pili.
VIKOSI:
Tottenham:Lloris 5,
Walker 5, Dawson 5, Vertonghen 6, Naughton 5 (Holtby 81), Dembele 5,
Paulinho 5, Townsend 6, Eriksen 5 (Soldado 74), Sigurdsson 5 (Lamela
63), Defoe 5.Subs: Friedel, Chiriches, Chadli, Sandro,.
Subs: Adrian, Jarvis, Petric, Maiga.
Goals: Reid 66, Vaz Te 72, Morrison 79
Ref: Lee Probert
No comments:
Post a Comment