Pamoja na AC Milan kupata Bao la kuongoza Sekunde 20 tu tangu Mechi ianze, Mabingwa Watetezi Juventus walizinduka na kuichapa AC Milan Bao 3-2 katika Mechi ya Serie A iliyochezwa Jana ndani ya Juventus Stadium huko Turin.
Sulley Muntari ndie aliefunga Bao la kwanza kwa AC Milan katika Sekunde ya 20 na Mkongwe Andrea Pirlo kusawazisha kwa Frikiki tamu katika Dakika ya 15.
Giovinco akaipa Juventus Bao la Pili katika Dakika ya 69, Dakika mbili tu baada kutokea Benchi, na Giorgio Chiellini kufunga Bao la 3 baada ya Frikiki ya Pirlo kupiga posti na kumrudia yeye.
AC Milan walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 74 baada ya Philippe Mexes kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu lakini Muntari aliwapoza kidogo kwa kuwafungia Bao la Pili, hilo likiwa Bao lake la Pili katika Mechi, na kuifanya Gemu iishe 3-2.
Ushindi huu wa Juventus umewafanya wafikishe Pointi 19 sawa na Napoli ambao wako Nafasi ya Pili kwa ubora wa Magoli, wote wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara AS Roma ambao Jumamosi waliitwanga Inter Milan 3-0.Mchezaji matata Sulley Muntari akifuahia bao lake la mapemaaa sana!! la sekunde 19.. (Dakika 1)
Pirlo akifunga frii kiki hapa na kusawazisha kufanya 1-1 kabla ya mapumziko!!
Kipa wa Milan Christian Abbiati hoi!! kwa bao la Pirlo!! chezea Pirlo wewe!
Sebastian Giovinco akifunga bao jingine na kufanya Juve iongoze ungwe
Aibu!! Philippe Mexes akioneshwa kadi nyekundu! kwa kufanya ndivyo sivyo uwanjani!
Giorgio Chiellini, Pirlo, wakipongezana kwa ushindi huku Muntari akimalizia bao la dakika za majeruhi dakika 90 ya mchezo kumalizika na kufanikisha 3-2.
No comments:
Post a Comment