BUKOBA SPORTS

Wednesday, November 20, 2013

ADEN RAGE ATEMWA NJE SIMBA!! YUMO NA KOCHA KIBADENI PAMOJA NA JULIO. WASIMAMISHWA KAZI NA KAMATI YA UTENDAJI SIMBA!

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku imemsimamisha Ismail Aden Rage kuendelea na ubosi katika klabu ya Simba na kulibadilisha benchi la ufundi isipokuwa nafasi ya meneja Madaktari wa timu ambapo pia kwa sasa wanamtarajia ZDRAVOK LOGARUSIC kutoka Croatia.

Akizungumza kwa niaba ya kamati ya utendaji, mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph Itangare amesema wamemsimamisha mwenyekiti kutokana na kufanya maamuzi yake binafsi bila kushirikisha kamati ya utendaji ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (1)ya katiba ya Simba.

Kingine alichosema Itangare ni ‘vilevile mwenyekiti huyo amesaini mkataba wa kukiuuza kipindi cha Simba tv bila kushirikisha kamati ya utendaji’


Kinesi amesema ‘Mwenyekiti tumemsimamisha lakini tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December’

‘Kutokana na timu yetu kutofanya vizuri, tumeamua kwamba benchi la ufundi tulifumue ili tulijenge upya, sasa litaongozwa na kocha aliekuwa na Gor Mahia ZDRAVOK LOGARUSIC amekubali kuja na ataanza mazoezi tarehe 2 Decemba na kwa pamoja tumekubaliana ndie atakuwa kocha mkuu, pia tumekubaliana Matola ndio awe msaidizi wake kwa muda, hatumuondoi Simba B moja kwa moja kuhofia kutetereka.


Baadaye tutakuletea taarifa za kina zaidi juu ya maamuzi hayo!

No comments:

Post a Comment