BUKOBA SPORTS

Wednesday, November 20, 2013

SWIDEN 2 v PORTUGAL 3, (Agg.2-4) CRIASTIANO RONALDO AIBEBA URENO!, AFUNGA HAT-TRICK NA KUIKIMBIZA URENO BRAZIL 2014 HUKU CRISTIANO RONALDO AKIMFUNIKA ZLATAN IBRAHIMOVIC!!

Cristiano Ronaldo alidhihirisha kwamba yeye ni Bora Duniani baada ya kupiga Bao 3 na kuiteketeza Sweden, wakiwa kwao, na kuipeleka Nchi yake Portugal kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Katika Mechi hii, Ronaldo aliipa Portugal Bao la kwanza lakini Zlatan Ibrahimovic akajibu mapigo kwa kuifungia Sweden Bao 2 za haraka na kuongoza Bao 2-1 na ndipo ‘Comandante’ Ronaldo alipoibuka na kupachika Bao 2 za haraka na kuipa Portugal ushindi wa Bao 3-2.
Washabiki wa Ronaldo wamempachika Jina la ‘Comandante’ kufuatia upuuzi wa Rais wa FIFA, Sepp Blatter, kumdhihaki Ronaldo na kumfananisha kama Kamanda wa Jeshi huku akimshabikia Lionel Messi.

Cristiano Ronaldo (kulia) akishangilia bao lake la tatu

Zlatan Ibrahimovic hoi kwa Ronaldo!!
Makali ya Cristiano Ronaldo yalifunika ubora wa Zlatan Ibrahimovic kwa kufunga bao 3 peke yake na kuisogeza Nchi yake kucheza Kombe la Dunia Brazil 2014.

Ronaldo akifunga bao dakika za mapema kipindi cha pili
Ibrahimovic na wenzie wakiwa hoi baada ya kufungwa bao la tatu na Cristiano!!!
Ibrahimovic akiachia mkwaju mkali wa friikiki!

Zlatan Ibrahimovic nyuma ya Ronaldo kwenye kamera! huku Ibra akiwa amefunga bao 2 tu
Zlatan Ibrahimovic akifunga bao kwa kichwa

Patashika golini!!

Ronaldo akisawazisha kwa kufanya 2-2 katika dakika ya 77 ya mchezo

Akifunga bao la tatu hapa!!

Ronaldo akifanya 3-2 na kufanya mabadiliko ya tangu mwanzo kuwa 4-2 Agg. na Portugal kusonga mbele

Cristiano Ronaldo Akipongezwa!
Cristiano Ronaldo akipongezwa tena hapa!!
VIKOSI:
Sweden: Isaksson, Lustig, Nilsson, Antonsson, Martin Olsson, Larsson (Gerndt 90), Elm (Svensson 45), Kallstrom, Kacaniklic (Durmaz 82), Elmander, Ibrahimovic.
Subs not used: Wiland, Jonas Olsson, Granqvist, Wernbloom, Bengtsson, Johansson, Toivonen, Zengin, Nordfeldt.
Booked: Olsson, Antonsson, Kallstrom, Svensson
Goals: Ibrahimovic 68, 72
Portugal: Rui Patricio, Joao Pereira, Pepe, Bruno Alves, Fabio Coentrao (Antunes 52), Meireles (Carvalho 73), Veloso, Joao Moutinho, Nani, Almeida (Ricardo Costa 82), Ronaldo.
Subs not used: Eduardo, Eder, Bruma, Luis Neto, Ruben Micael, Varela, Josue, Postiga, Beto.
Booked: Nani
Goals: Ronaldo 50, 77, 79

No comments:

Post a Comment