BUKOBA SPORTS

Saturday, November 30, 2013

CARDIFF CITY 0 v ARSENAL 3, AARON RAMSEY NA FLAMINI WAIPANDISHA ZAIDI KILELENI GUNNERS RAMSEY AKITUPIA MBILI. MZEE WENGER AUKUBALI MUZIKI WA VIJANA WAKE!!

CARDIFF CITY 0 v ARSENAL 3
LEO kwenye ligi kuu England Arsenal wakicheza huko Ugenini Cardiff, Bao mbili za Aaron Ramsey na moja la Mathieu Flamini zimewapa Arsenal ushindi wa Bao 3-0 walipocheza Ugenini na Cardiff City.
Ushindi huu umewafanya Arsenal wazidi kupaa kileleni wakiwa Pointi 7 mbele.
Kocha Malky Mackay na Arsene Wenger wakiteta jambo kabla ya mtanange kuanzaOlivier Giroud kulia akikabwa na mchezaji wa Cardiff leo hii jioni kwenye ligi kuu.Kim Bo-Kyung akijaribu kumtoka Mesut OzilJuu ya lango!! Chupuchupu!!Ramsey akitupia bao la kufungua la kwanza kwa timu yake Gunners!Kipa David Marshall hakuona ndani!!Angalia staili ya kushangilia bao baada ya Ramsey kufunga bao ...ni full kupongezana!Kupongezana ni muhimu!!Ramsey akitupia la pili...Mpaka nyavuni...!Flamini akizichoma nyavu za Cardiff baada ya kutengewa na Mesut OzilFlamini akishangilia bao lakeMajanga kwa kipa!!Ramsey akisalimia mashabiki kwenye uwanja wa Cardiff baada ya mpira kumalizika, Gunners wakiwa mbele vifua wazi kwa ba0 3-0 dhidi ya wenyeji Cardiff.

MATOKEO/RATIBA
Jumamosi Novemba 30
Aston Villa 0 Sunderland 0
Cardiff 0 Arsenal 3
Everton 4 Stoke 0
Norwich 1 Crystal Palace 0
West Ham 3 Fulham 0 

Newcastle 2 v West Brom 1

RATIBA: 
Jumapili Desemba 1
15:00 Tottenham v Man United
17:05 Hull v Liverpool
19:10 Chelsea v Southampton
19:10 Man City v Swansea

No comments:

Post a Comment