BUKOBA SPORTS

Friday, November 22, 2013

EBSS FAINALI NOVEMBA 30

Ziku chache zimebaki ile shindando kubwa kabisa hapa Tanzania la Epic Bongo Star Search (EBSS) kufanyika, litarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba 30 mwaka huu katika jiji la Dar es Salaam katika Ukumbi wa Escape 1. 

Kuna washiriki wapatao 6 waliotinga katika fainali hizo, nao ni Mandela Nicolaus (10), Emmanuel Msuya (21), Melisa John (22), Amina Chibaba (03), Elizabeth Mwakijambile (08) Maina Thadei. Na washiriki hawa sita walioingia katika kinyang'anyilo cha fainali watatakiwa kuimba nyimbo walizotunga wenyewe siku hiyo ya fainali.

Mkurugenzi wa Benchmark Production Bi. Rita Paulsen, alisema kuwa wameamu kuja kitofauti zaidi mwaka huu ili kuboresha shindano hilo, ambalo huu ni mwaka wake wa saba tangu kunzishwa kwake. Kaa tayari kumjua mshindi wa mwaka huu ni nani kati ya hao sita atakaye ondoka na kitita cha 50,000,000/= za kitanzania.


No comments:

Post a Comment