BUKOBA SPORTS

Thursday, November 21, 2013

KUNDI LA TOTOJI MAZINGE MABINGWA MBIO ZA MITUMBWI UKEREWE, TIKETI MKONONI NA TAYARI KUCHUANA KWENYE FAINALI JIJINI MWANZA DECEMBER 7.2013

KUNDI la wapiga kasia Wanaume (pichani juu) lililo ongozwa na nahodha Totoji Mazinge Ngoroma kutoka wilayani Ukerewe limetwaa ubingwa wa mashindano ya mbio za Mitumbwi zinazo dhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini TBL kupitia Bia ya Balimi na hivyo kujitwalia zawadi ya fedha taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe katika mashindano ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza hivi karibuni.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na kundi lililoongozwa na nahodha Toto Sebastian likizoa kitita cha fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe katika fainali za Kanda jijini Mwanza ,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kundi la nahodha Simon Fundi lililojinyakulia fedha taslimu shilingi 500,000/=


Upande wa Wanawake kundi lililoongozwa na mwanamama Mhete Muhoja lilitwaa ubingwa na hivyo kuzawadaiwa fedha taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe kwenye mashindano ya Kanda.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na kundi lililoongozwa na nahodha Jenifer Elias lijinyakuliwa fedha taslimu shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha kisiwa hicho kwenye fainali za Kanda jijini Mwanza, nafasi ya tatu ilichukuliwa na kundi la nahodha Edna Chambo lililozawadiwa fedha taslimu shilingi 400,000/=

Akizungumza na wananchi waliofurika kwa wingi katika ufukwe wa Monarch Galu Beach meneja mauzo wa TBL wilaya ya Ukerewe, Josephat Changwe amesema kuwa licha ya mchezo huo kuwa burudani kampuni yake imenuia kuyaboresha mashindano hayo ili yapate sura ya kimataifa huku yakibadili maisha ya wananchi kama sehemu ya mitaji.

Mmoja kati ya waratibu wa michuano hiyo wilaya ya Ukerewe akiwakagua na kuwapanga washiriki wa mbio za mitumbwi wanaume.

Wananchi wakubwa kwa wadogo walijitokeza kushuhudia mashindano hayo.

Jamaa ambaye alikuwa kapteni wa moja ya kundi washiriki wanaume aliamua kujipigilia vazi hili kutia ladha ambapo mwisho wa siku kundi lake liliambulia nafasi ya 5 na kupata kifutajasho cha shilingi laki mbili.

Kwa mkwara wengine walitinga sketi kama anavyoonekana jamaawa kwanza kushoto mstari wa mbele.

K Mseleche Katibu Tawala wa wilaya ya Ukerewe akifungua mashindano ya mbio za mitumbwi kwa wilaya ya Ukerewe, kulia kwake mwenye kaunda suti ya bluu ni Mwenyekiti wa Mashindano ya Mbio za makasia nchini Mr. Mugabo.

Hivi ndivyo mbio zilivyoanza ambapo kwa upande wa wanaume yalikimbia makundi matatu kwa awamu tofauti na kisha baadaye ikapigwa fainali kwa vinara wa tano wa kila kundi kumpata bingwa na nafasi nyingine.

Waleeee....

Licha ya mashindano haya kuwa mchezo unaopendwa pia yamegeuka kuwa sehemu ya kivutio cha utalii.

Mtalii akijumuika kucheza ngoma ya asili ya Kikerewe.

watu walifurika katika mwalo huu wa burudani wa Galu Beach.

Na sasa ikawa zamu ya washiriki upande wa wanawake.

Watazamaji...

Kundi mabingwa upande wa wanawake lililoongozwa na nahodha wake Mhete Muhoja likiwasili ufukweni kushika nafasi ya kwanza ambapo lilinyakuwa fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe kwenye mashindano ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 7 disemba 2013 jijini Mwanza.

Kundi la nahodha Jenifer Elias likiufikia ukingo wa mashindano kuinyakuwa nafasi ya pili, fedha taslimu shilingi 600,000/= pamoja na nafasi kuwakilisha kisiwa cha Ukerewe kwenye fainali za Kanda jijini Mwanza.
Fainali za Kanda za mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Decemba 7, 2013, katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo watashindana mabingwa wa Kanda nzima ambao ni kutoka Kigoma, Kagera,Ukerewe,Musoma na wenyeji Mwanza.

No comments:

Post a Comment