Mchezaji wa Ajax Danny Hoesen akishangilia pamoja na Davy Klaassen baada ya kuifunga bao Barca
Hoesen akiachia shuti kali lililompita mlinda mlango wa BarcelonaViktor Fischer akishangilia kwa aina yake na huku akiwa amevua jezi!!
Kocha wa Barcelona Gerardo 'Tata' Martino amekiri kwamba timu yake ililegeza kamba katika mchezo kati yake na Ajax kwa kuamini kwamba tayari imefuzu katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa ambapo kwa mara ya kwanza wamepoteza mchezo mmoja msimu huu baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa timu ya Ajax jana Jumanne.
Mchezaji wa Barcelona Neymar akikabwa vilivyo na Joel Veltman
Barcelona ilichakazwa na wenyeji wa mchezo huo Ajax katika nusu ya kwanza ya mchezo wakati magoli kutoka kwa Thulani Serero na Danny Hoessen kuifanya timu yao kuongoza kwa magoli 2-0.
Katika kipindi cha pili Barcelona ilipata nafasi ya kuweza kufufuka na kusawazisha magoli hayo katika dakika za mwanzoni za kipindi hicho wakati Joel Veltman alipotolewa nje kwa kumchezea vibaya Neymar ndani ya eneo la hatari na Xavi kupunguza nusu ya magoli kwa kufanikiwa kutikisa nyavu za Ajax na kuiandikia timu yake goli moja.
Hata hivyo pamoja na Ajax kuwa na wachezaji 10 pekee, Barcelona ilishindwa kupata sare na hivyo kujikuta wameangukia pua kwa mara ya kwanza katika michezo 21 waliyoicheza tangu Martino alipoanza kukionoa kikosi hicho.
Bamoja na matokeo hayo Barcelona bado inaendelea kuongoza katika kundi H na inahitaji alama moja dhidi ya Celtic,katika mchezo wa fainali huko Camp Nou ili kuhakikisha kwamba inamaliza ya kwanza katika kundi hilo.
No comments:
Post a Comment