Jesús Navas 1' • Sandro 34' OG • Sergio Agüero 41' • Sergio Agüero 50' Álvaro Negredo 55' Jesús Navas 90' +2' • Manchester City leo wameinyuka timu ya Tottenham Hotspurs bao 6-0 kwenye uwanja wa Etihad. City wakitandaza soka safi na wakionesha kiwango chao cha hali ya juu nyumbani kwao ndio walionza kupata bao la mapema dakika ya 1 baada ya mchezaji wao mpya Jesús Navas kufunga bao hilo. City waliongeza bidii zaidi ili wajikwamue watoke nafasi waliokuwa nayo nafasi ya tisa baada ya kufungwa na vibonde Sunderland wiki iliyopita.
Bao la pili la Manchester City limefungwa dakika ya 34 kwa mchezaji Sandro kujifunga bao hilo baada ya kucheza ndivyo sivyo, Bao la tatu likifungwa na Sergio Agüero dakika 41 na akifunga tena bao jingine la pili dakika ya 50, Álvaro Negredo akafunga bao tena kwa City katika dakika ya 55.
Jesús Navas akawafunga bao tena Spurs katika dakika za lala salama dakika ya 90' +2.
Ushindi huu unawapandisha City hadi nafasi ya NNE wakiwa na Alama 22.
Jesus Navas akiifungia bao Man City dhidi ya Tottenham katika dakika ya 1
Sandro akijifunga bao hapa baada ya Alvaro Negredo kuachia shuti
Kipa wa Spurs Hugo Lloris akianga Sergio Aguero akitupia ndani ya lango lake mpira muda mchache kabla ya mapumziko
Negredo akituliza mpira kwa makini na kuachia shuti kali.
Negredo akipongezwa na Aguero pamoja na Samir Nasri baada ya kufunga bao la nne
Jan Vertonghan akimkaba Navas jambo ambalo halikuwezekana katika dakika za lala salama na shuti kali la Navas kuingia langoni mwao.
VIKOSI:
Man City: Pantilimon 6; Zabaleta 7,
Demichelis 6, Nastasic 6 (Lecsott 45mins 6), Clichy 6; Toure 7,
Fernandhino 7; Navas 7, Negredo 8, Nasri 8 (Milner 77mins 6); Aguero 8
(Garcia 69mins 6).Subs not used: Hart, Richards, Dzeko, Guidetti.
Scorers: Navas, 1, 90, Aguero 41, 51, Sandro og 34, Negredo 56.
Booked: Toure.
Subs not used: Friedel, Chiriches, Townsend, Defoe.
Booked: Walker, Vertonghen, Sandro.
Referee: Howard Webb
Attendance: 47,228
No comments:
Post a Comment