Danny Graham akiwaomba pole mashabiki wa Swansea baada ya kuipatia bao Hull
Mechi pekee ya Ligi Kuu England iliyochezwa Jana Usiku, Swansea City na Hull City zilitoka Sare ya Bao 1-1.
Danny Graham, ambae alitokea Swansea, katika Dakika ya 9 alimaliza ukame wa Mechi 30 bila Goli, alipoifungia Hull Bao lao alipounganisha krosi ya Ahmed Elmohamady anaetoka Egypt.
Swansea walisawazisha katika Dakika ya 60 kwa Bao la Chico Flores toka krosi ya Jonjo Shelvey.
No comments:
Post a Comment