BUKOBA SPORTS

Thursday, December 12, 2013

NAHODHA STEVEN GERRARD NJE MWEZI MMOJA!

Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard atakuwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mmoja baada ya kuumia Misuli za Pajani Jumamosi iliyopita kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo Liverpool waliifunga West Ham Bao 4-1.
Habari za kuumia na kuwa nje kwa muda huo mrefu zimethibitishwa na Klabu ya Liverpool baada ya Mchezaji huyo kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Hili ni pigo kwa Liverpool ambao pia kwa sasa wanamkosa Straika wao mahiri Daniel Sturridge ambae pia ni majeruhi na ambae atakuwa nje kwa Miezi miwili baada kuumia enka.

Habari hizi zitawasumbua sana Liverpool maana ndio wanaingia kwenye kipindi cha Mechi nyingi na mfululizo na Jumapili wanaanza Ugenini kucheza na Tottenham kisha kucheza Nyumbani na Cardiff City na kufuatia Mechi za Ugenini dhidi ya Manchester City na Chelsea, zote zikiwa kabla ya mwisho wa Mwezi huu.
Kwa sasa Liverpool wapo Nafasi ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi, wakiwa Pointi sawa na Chelsea na kuwazidi Magoli tu, na wako nyuma ya Vinara Arsenal kwa Pointi 5.

No comments:

Post a Comment