UEFA CHAMPIONS LIGI, Usiku huu imemaliza hatua ya Makundi na kutoa Timu 16 ambazo Jumatatu ijayo zitaingizwa kwenye Droo kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Vinara wa Ligi Kuu England, Arsenal, walipigwa Bao 2-0 na Napoli huko Italy lakini hilo halikutosha kwa Klabu hiyo ya Serie A kwani ilijikuta ikimaliza Nafasi ya Tatu katika Kundi F baada ya Borussia Dortmund kuichapa Marseille Bao 2-1 huko France.
Matokeo hayo yameifanya Dortmund kutwaa Nafasi ya kwanza ya Kundi F na kuiacha Arsenal ikiwa Nafasi ya Pili na sasa ipo hatarini kupambana na mmoja wa Vigogo wa Ulaya katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Katika Raundi hiyo, Arsenal inaweza ikakutana na mmoja kati ya Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, PSG au Atletico Madrid.
NAPOLI 2 v ARSENAL 0
Napoli waliichapa Arsenal Bao 2-0 lakini wakajikuta hawakufuzu kwani Borussia Dortmund, wakicheza Ugenini, waliichapa Marseille Bao 2-1. Kwa Matokeo haya, Kundi F, Mshindi wa Kwanza ni Borussia Dortmund na wa Pili ni Arsenal, ambao ndio watasonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Napoli kutupwa EUROPA LIGI kwa kumaliza Nafasi ya Tatu. Bao la kwanza la Napoli lilifungwa na Gonzalo Higuain na Arsenal kujikuta wako Mtu 10 baada Mikel Arteta kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 76.
Bao la Pili la Napoli lilifungwa katika Dakika za Majeruhi na Jose Callejon na kuifanya Napoli iwe mbele kwa Bao 2-0 lakini hilo halikutosha kwao kwani Dortmund walifunga Bao la ushindi katika Dakika ya 87 kupitia Kevin Grosskreutz walipoifunga Marseille Bao 2-1 huko France.
Kwenye Mechi hiyo Robert Lewandowski ndie aliewapa Dortmund Bao la Kwanza katika Dakika ya 4 na Marseille kusawazisha kwa Bao la Diawara la Dakika ya 14 lakini katika Dakika ya 34 Payet alipewa Kadi Nyekundu na kuwaacha Marseille wakiwa Mtu 10.
Katika Mechi ya Napoli na Arsenal, endapo Napoli wangepata Bao la 3, basi Arsenal wangetupwa EUROPA LIGI.Arteta alitolewa nje kwa kadi nyekundu hivyo atakosa mchezo wa kwanza wa hatua ya 16.Tomas Rosicky chini Pandev akigonga mpira kwa kichwaMathieu Flamini na Blerim Dzemaili wakichuanaGonzalo Higuain akipelekeshwa chini hapaOlivier Giroud akikingwa kwa kuzuiliwa uso hapa na mchezaji wa Napoli kushotoWenger na Benitez wakitazama kwa makini vijana wao.

Mapema timu zote mbili zilimwombea Nelson Mandela kabla ya mtanange.
No comments:
Post a Comment