Arsenal wameshinda Mechi 4 kati ya 5 za Kundi F, ambalo hadi sasa halijatoa Timu iliyofuzu, lakini bado hawana uhakika wa kusonga na Jumatano wapo Ugenini huko Italy wakitakiwa wapate Sare tu ili wafuzu.
Wenzao Chelsea, ambao wameshafuzu toka Kundi E, wanachowania ni kushinda uongozi wa Kundi hilo ili kujihakikishia kile kinachosemwa ‘ubwete’ kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Napoli boss Rafael Benitez (ambaye hayupo pichani) ambaye timu yake leo usiku itacheza na timu ya Arsenal anayoongoza Mzee Arsene Wenger kwenye UEFA Champions ambapo pia kocha huyo ameweka bayana kuwa kiwango cha Gunners ni kizuri na wanaweza kutwaa kombe msimu huu wa 2013/2014.
Wachezaji wa Napoli wakifanya mazoezi.
RATIBA: LEO JUMATANO
Jumatano 11 Desemba 2013
Schalke 04 v FC Basel
Chelsea FC v FC Steaua Bucureşti
Olympique de Marseille v Borussia Dortmund
Napoli v Arsenal FC
FK Austria Wien v Football Club Zenit
Club Atlético de Madrid v FC Porto
AC Milan v AFC Ajax
Barcelona v Celtic FC
KUNDI E Chelsea imefuzu, bado moja |
|||||||||
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Chelsea | 5 | 3 | 0 | 2 | 11 | 3 | 8 | 9 |
2 | FC Basel 1893 | 5 | 2 | 2 | 1 | 6 | 5 | 1 | 8 |
3 | Schalke | 5 | 2 | 1 | 2 | 4 | 6 | -2 | 7 |
4 | FC Steaua Bucuresti | 5 | 0 | 1 | 2 | 2 | 9 | -7 | 3 |
FC Basel watasonga pamoja na Chelsea ikiwa tu hawafungwi na Schalke leo usiku.
KUNDI F Hamna iliyofuzu |
|||||||||
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Arsenal | 5 | 4 | 0 | 1 | 8 | 4 | 4 | 12 |
2 | BV Borussia Dortmund | 5 | 3 | 0 | 2 | 9 | 5 | 4 | 9 |
3 | Napoli | 5 | 3 | 0 | 2 | 8 | 9 | -1 | 9 |
4 | Olympique de Marseille | 5 | 0 | 0 | 5 | 4 | 12 | -8 | 0 |
Arsenal watasonga tu ikiwa watakwepa kipigo kikubwa Ugenini na Napoli lakini pia ikiwa Borussia Dortmund itashindwa kuifunga Marseille, Arsenal watapita tu hata wakibondwa kwa Bao nyingi na Napoli.
Napoli wako sawa na Borussia Dortmund, na ili wao kufuzu kwa mujibu wa kanuni za UEFA kufuatia matokeo ya Uso kwa Uso, wanahitaji kumaliza wakiwa na Pointi zaidi kupita Dortmund.
No comments:
Post a Comment