FAINALI ya CHALENJI CUP itakuwa kati ya Wenyeji Kenya na Sudan baada ya jana kuzibwaga Kilimanjaro Stars na Zambia kwenye Nusu Fainali.
Kenya waliifunga Kilimanjaro Stars Bao 1-0 katika Mechi iliyohamishwa toka Machakos na kupelekwa Nyayo Stadium, Nairobi baada ya Uwanja kufurika maji.
Hata kuko Nyayo Stadium, Mechi hiyo ilichezwa kwenye mvua na Kenya kufunga Bao lao la ushindi katika Dakika ya 4 kwa Bao la Clifton Miheso.
Katika Nusu Fainali nyingine, Zambia na Sudan zilitoka 0-0 katika Dakika 90 na Mechi kuongezwa Dakika 30 ambapo Sudan walishinda 2-1.
Zambia walitangulia kufunga katika Dakika ya 110, Mfungaji akiwa Ronald Kampamba na Sudan kusawazisha Dakika ya 114 kwa Bao la Miaaz Abdelrahim na kupata Bao la usjindi kwenye Dakika ya 118 lililofungwa na Salah Ibrahim.
Mechi za kusaka Mshindi wa Tatu, kati ya Kilimanjaro Stars na Zambia, na Fainali, kati ya Kenya na Sudan, zote zitachezwa Nyayo Stadium hapo Desemba 12.
Kenya waliifunga Kilimanjaro Stars Bao 1-0 katika Mechi iliyohamishwa toka Machakos na kupelekwa Nyayo Stadium, Nairobi baada ya Uwanja kufurika maji.
Katika Nusu Fainali nyingine, Zambia na Sudan zilitoka 0-0 katika Dakika 90 na Mechi kuongezwa Dakika 30 ambapo Sudan walishinda 2-1.
Zambia walitangulia kufunga katika Dakika ya 110, Mfungaji akiwa Ronald Kampamba na Sudan kusawazisha Dakika ya 114 kwa Bao la Miaaz Abdelrahim na kupata Bao la usjindi kwenye Dakika ya 118 lililofungwa na Salah Ibrahim.
Mechi za kusaka Mshindi wa Tatu, kati ya Kilimanjaro Stars na Zambia, na Fainali, kati ya Kenya na Sudan, zote zitachezwa Nyayo Stadium hapo Desemba 12.
No comments:
Post a Comment