Timu ya Galatasaray wakicheza kwao Türk Telekom Arena Ali Sami Yen Spor Kompleksi Mjini Istanbul, leo
wameifunga Juventus Bao 1-0 katika Mechi ya Kundi B la UCL, UEFA
CHAMPIONS LIGI, iliyovunjika Jana baada Uwanja kufunikwa na Barafu baada
ya Dakika 31 na kuendelea kuchezwa leo kwa Dakika 59 zilizobaki.
Hata hii leo, Mechi ilichezwa katika mazingira magumu maana Barafu iliendelea kuanguka na Uwanja kuonekana mbovu na kujaa matope kwa sehemu nyingi.
Bao la ushindi la Galatasaray lilifungwa na Wesley Sneijder katika Dakika ya 85 baada ya kupokea pasi ya kichwa ya Didier Drogba alieshusha Mpira huo kufuatia pasi ya juu toka nyuma.Wakati Juve wakihitaji Sare tu ili kuungana na Real Madrid kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Galatasaray walitakiwa lazima washinde na Sneijder amewafanya waungane na Real na kuwaacha Juve waende kucheza EUROPA LIGI.
Wachezaji wakisepa kwenda kwenye vyumba vyao baada ya kucheza dakika 31 bila kufungana baada ya kufunikwa na Barafu
Mechi ilibidi imalizike leo na hata hivyo Barafu leo lilikuwepo la kiaina!
Msimamo ulivyo Juventus wakishika nafasi ya tatu na zikiwa zinahitajika timu mbili tu, hivyo Juve wametupwa kucheza Europa Ligi.
Wakijaribu kupunguza Barafu uwanjani
Hata hivyo walivyokuwa wakiendelea kupunguza barafu jingine lilikuwa linamwagika nyuma yao walipokuwa wanamaliza
MSIMAMO:
KUNDI B -IMEFUZU: Real Madrid |
|||||||||
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Real Madrid CF | 6 | 5 | 1 | 0 | 20 | 5 | 15 | 16 |
2 | Galatasaray Spor Kulübü | 6 | 2 | 1 | 3 | 8 | 14 | -6 | 7 |
3 | Juventus | 6 | 1 | 3 | 2 | 9 | 9 | 0 | 6 |
4 | FC Copenhagen | 6 | 1 | 1 | 4 | 4 | 13 | -9 | 4 |
No comments:
Post a Comment