Shirikisho la kandanda nchini Afrika ya kusini SAFA limeungana na raia nchini humo na ulimwengu mzima kuomboleza kifo cha raisi wa kwanza mzalendo na muasisi wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela aliyeaga duania usiku wa Alhamisi.
R.I.P Nelson Mandela
Mandela alifikwa na mauti akiwa nyumbani kwake Houghton mishale ya saa tatu kasoro za usiku kwa saa za Afrika ya kusini.
Raisi wa shirikisho la kandanda nchini humo Danny Jordaan amemwelezea Madiba kuwa aliwajibika sana kuinua ari ya uzalendo katika mchezo wa kandanda hususan katika mazungumzo yaliyoleta chachu ya ushondi wa kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1996.
Enzi hizo!!
Mandela alichochea ari na jitihada za timu ya Afrika ya kusini kukabiliana na mchuano wa Kombe la Dunia mwaka 2010.
Jordaan ameongeza kuwa kuzorota kwa hali ya afya ya Mandela katika kipindi cha mwaka jana kuliwashtua.
Shirikisho la kandanda nchini Afrika ya kusini SAFA na jumuiya ya kandanda zimetoa wito wa kutoa heshima kwa hayati Nelson Mandela kwa kukaa kimya kwa sekunde kadhaa katika kila mechi itakayochezwa ikiashiria heshima kwa kiongozi huyo aliyeamsha hisia za kizalendo ndani ya taifa hilo. Quai d'Orsay Foreign Affairs Ministry in ParisWaombolezaji wakiomboleza kifo cha Nelson Mamndela huko Africa Kusini leoBaada ya kuugua kwa muda mrefu Mwili wa Nelson Mandela ukiwa kwenye gari maalum huko Africa Kusini
No comments:
Post a Comment