Manchester United leo wamepata kipio chao cha pili mfululizo cha Ligi Uwanjani kwao Old Trafford na hii ni mara ya kwanza tangu Mwaka 2002 wakati Newcastle waliposhinda Bao 1-0 na hii ni mara ni mara ya kwanza kwa Newcastle kushinda Uwanjani hapo tangu Mwaka 1972.
Bao la ushindi la Newcastle lilifungwa na Yohan Cabaye katika Dakika ya 61.
Man United, ambao leo walibadilisha Wachezaji 7 toka Kikosi kilichofungwa Jumatano, walipata nafasi kadhaa za kufunga pale Patrice Evra alipopiga kichwa na Mpira kupiga posti na nyingine ni majaribio ya Javier Hernandez na Adnan Januzaj yaliyookolewa na baadae Bao la Robin van Persie kukataliwa kwa kuwa Ofsaidi.
Jumatano iliyopita Man United walifungwa Old Trafford na Everton Bao 1-0 na Mechi inayofuata kwao ni hapo Jumanne Desemba 10 watakapocheza UEFA CHAMPIONS LIGI Uwanjani Old Trafford na Shakhtar Donetsk.
Wachezaji wa Newcastlewakimpongeza mchezaji mwenzao Cabaye baada ya kuifunga United bao katika dakika ya 61 kipindi cha pili.
Wachezaji Manchester United hoi!!! akiwemo Robin van Persie na wengineo!!
Van Persie alijaribu kufunga bao hapa na mwamuzi akadai alikuwa ameotea!!
David Moyes akiteta na Hatem Ben Arfa
Leo tenaaaaaa!!!! kichapo!!! David Moyes akiingia kwenye uwanja wa Old Trafford
Juhudi: Fabricio Coloccini akiondosha mpira kwa Adnan Januzaj
Mapema: Kocha David Moyes akipiga makofi na kuomba kwa sala kwa kifo cha aliyekuwa Rais wa Zamani mweusi wa Africa kusini Bw. Nelson Mandela!
VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra, Nani (Zaha 68), Cleverley (Anderson 69), Jones, Januzaj, Van Persie, Hernandez.Newcastle: Krul, Debuchy, Williamson, Coloccini, Santon, Cabaye, Tiote, Anita, Sissoko, Remy, Gouffran (Ben Arfa 57).
Goal: Cabaye 61.
No comments:
Post a Comment