BUKOBA SPORTS

Saturday, December 7, 2013

U20: TANZANITE 1 vs SOUTH AFRICA 4, BASETSANA YAFANYA KWELI LEO TAIFA!!


Ubao ukiteta zaidi..

Timu zote mbili pamoja na waamuzi wakiingia uwanjani
Wachezaji pande zote mbili wakisalimiana muda mfupi kabla ya mtanange kuanza

Kikosi kilichoanza cha Africa kusini
Kikosi cha Tanzanite

Wakisamiana timu kapteini

Wachezaji wa akiba wa Africa kusini

Afrika kusini wakishangilia bao dakika ya 13

Mchezaji wa Tanzanite akiondosha mpira mbele

Katika kukabana hapa

Patashika kwenye lango la Africa Kusini

Mchezaji wa Tanzanite akitaka kumtoka mchezaji wa Afrika kusini

TIMU ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 Tanzania 'Tanzanite' imefungwa mabao 4-1 na Afrika Kusini 'Basetsana' kwenye mchezo wa raundi ya pili ya kutafuta nafasi ya kufunzu kombe la dunia mwakani nchini Canada kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Afrika Kusini ilianza vyema mchezo huo kwa kuwazidi ujanja Tanzanite katika kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya kuzitumia vizuri nafasi walizopata kwa kufunga bao la kwanza dakika ya nne ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Amogelang Motay.
Bao hilo liliamsha mashambulizi makali kwa Tanzanite waliokuwa wakitafuta nafasi ya kusawazisha ambapo dakika ya 13 walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Theresa Yohana alimpiga shuti la mita kama 30 na kuingia golini moja kwa moja.
Mashambulizi yaliendelea pande zote mbili, ambapo dakika ya 17 mchezaji wa Afrika Kusini Shiwe Nogwanya aliipatia timu yake bao la pili lililodumu hadi mapumziko.

Baada ya mapumziko timu zote zilikuwa zikifanya mashambulizi lakini Afrika Kusini waliendeleza mashambulizi yao upande wa Tanzanite na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa mchezaji wake Mosili Makhoali dakika ya 61. Uzoefu wa Afrika Kusini ulionekana dhahiri kwani waliliandama lango la Tanzanite kila mara lakini golikipa Najiat Abbas alikuweza kupangua mashuti kadhaa na mengine kuishia nje lakini uzembe wa mabeki uliweza kusababisha kufungwa bao la nne dakika ya 78 kupitia kwa Mosil Makhoali.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Waziri wa habari, vijana michezo na Utamaduni, Fenella Mukangara aliwataka wachezaji kutolia kwani mwanamke jasiri anapanga nini afanye baada ya alichotangulia kukifanya hivyo kwa pamoja na benchi la ufundi wakae watathimini walipokosea ili wafanye marekebisho kwa ajili ya mchezo wa marudiano

No comments:

Post a Comment