
Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal na Barcelona Thierry Henry amesema angependelea kumuona winga wa Bayern Munich Frank Ribery akishinda tunzo ya Ballon d'Or this year.


"Ribery ni mchezaji mkubwa na mwenye haiba ya kipekee anapokuwa uwanjani" Henry alikuwa akiongea na Sky Sports.
"anafikiria zaidi kutengeneza magoli kuliko kujitengenezea magoli.Ni aina ya mchezaji ambaye unapenda kucheza naye, napenda ashinde tuzo."
Ribery anakabiliana na ushindani kutoka kwa wakali wengine wa kufumania nyavu kutoka ligi ya Hispania Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
No comments:
Post a Comment