BUKOBA SPORTS

Saturday, December 14, 2013

YANGA YAPETA LEO YAIFUNGA 3-2 TIMU YA KMKM KWENYE UWANJA WA TAIFA

MABNGWA wa soka wa Tanzania Bara Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya KMKM kutoka Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo.

Yanga iliutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi Januari na mechi ya mtani jembe baina ya timu hiyo na hasimu wake mkubwa Simba itakayochezwa katika Uwanja wa Taifa Jumamosi ijayo.






Kwenye wa jana Yanga ilicheza bila ya nyota wake wa kikosi cha kwanza waliokuwa na timu zao za taifa kwenye mashindano ya kombe la Chalenji yaliyofanyika Nairobi, Kenya na wenyeji kunyakua taji hilo kwa kuifunga Sudani kwenye mchezo wa fainali.
Nyota hao ambao hawakuwa na Yanga kwenye mchezo wa jana ni pamaja na kiungo Athumani Idd’Chuji’, kipa Deogratius Munishi’Dida’, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga waliokuwa na Kilimanjaro Stars.


Yanga pia haikuwa na kiungo wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima na mshambuliaji Khamisi Kiiza wa Uganda waliokuwa na timu zao za taifa kwenye mashindano hayo ya Nairobi.

Yanga waliotawala sehemu kubwa ya mchezo huo hasa kipindi cha kwanza iliandika bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Jerry Tegete kwenye dakika.

Mbali na bao hilo Yanga walipoteza nafasi nyingi za kufunga kipindi hicho mbili zikipotezwa na kiungo wake chipukizi Relient Lusajo kwenye dakika ya 27 na 29 na beki wa kushoto wa timu hiyo David Luhende alikosa bao la wazi kwenye dakika ya 37.


KMKM walikaribia kusawazisha kwenye dakika ya 52 lakini shuti la mshambuliaji wa zamani wa Simba Ally Shiboli lilipaa juu ya lango la Yanga lililokuwa linalindwa na kipa Juma Kaseja ukiwa mchezo wake wa kwanza baada ya kurejea tena kwenye timu hiyo aliyojiunga nayo mwaka 2010 akitokea Simba.


Tegete alipoteza nafasi nzuri ya kufunga akiwa peke yake na kipa wa KMKM Mudathiri Khamisi na kocha wa Yanga aliwapumzisha Nadir Haroub’Cannavaro’, Oscar Joshua na Jerry Tegete na Didier Kavumbagu na kuwaingiza Rajabu Zahiri, Shaabani Kondo, Saidi Bahanunzi na Hussein Javu.


Baada ya mabadiliko hayo Yanga walionekana kupoteana hali iliyosababisha KMKM kufunga bao la kwanza lililofungwa na Faki Ali na Shiboli alifunga bao la pili kwenye dakika ya 72.


Huku ikidhaniwa kuwa KMKM walau wangeondoka na sare kwenye mechi hiyo kiungo chipukizi wa Yanga Khamis Thabiti aliifunga bao la tatu kwa shuti kali kwenye dakika ya 83 akiwa nje ya eneo la penalti.

No comments:

Post a Comment