
Tottenham wamepindua kipigo cha Bao 1-0 walichopata huko Ukraine na kuichapa FC Dnipro Bao 3-1 na wao kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EUROPA LIGI.
Bao za Tottenham zilifungwa na Sandro, Dakika ya 45 na FC Dnipro kusawazisha Dakika ya 47 kwa Bao la Zozulja lakini Adebayor akapiga Bao 2 katika Dakika za 65 na 69 na kuipa Tottenham ushindi.
FC Dnipro walipata pigo Dakika ya 63 baada Mchezaji wao Zozulja kupewa Kadi Nyekundu.
Jermain Defoe nae alikuwepo kushuhudia kipute hicho!

Patashika kuutafuta mpira..

Chupuchupu Soldado afunge bao mapema..

Dnipro wakifunga bao lakini baadae walipotea na kufungwa na kuondolewa nje ya michuano hiyo!

Zozulya akitofautiana na Jan Vertonghen na hapa walipandishiana

Majanga Uwanjani!! mbele ya Mwamuzi...

Wazi wazi ...kweupe!!

Michael Dawson chini...

Taswira Michael Dawson akiwa chini na wengine wakiwa wanakwaruzana katika fujo za hapa na pale!!!

Onyo!! Mwamuzi na Kocha wa Muda wa Spurs wakinyoosheana kidole!! ....swala ni kufanya haki!
Sawa...sikatai...mtoe nje sasa!!!

Mwamuzi Anthony Gautierakimtoa nje Zozulya

Kilichofata ni kipigo kwa timu ya Fc Dnipro

Spurs wakifanya 2-2 Agg:

Mtajiju ....twende nikawafunge!!

Bao....

Adebayor akionesha saluti baada ya kuinyonga FC DNIPRO

Safi....Adebayor...

Adebayor akiteta kimya kimya na mashabiki wa Spurs!! raha ya kufunga bao

Defoe

Kutoka kwenye ushindi mpaka kutupwa nje

kupumua kwa shida!!!!!
No comments:
Post a Comment